Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa leo ametembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na kueleza dhamira ya Serikali kuyafanya makazi hayo kuwa kituo cha utalii.
Akizungumza akiwa nyumbani kwa Baba wa Taifa katika eneo la Mwitongo, Kijiji cha Butiama, Mheshimiwa Majaliwa amemuagiza Mkuu wa Wilaya ya Butiama Mhe. Moses Kaegele kutembelea na kulikagua mapungufu yaliyopo katika eneo hilo ili Serikali iweze kuboresha makazi hayo.
Aidha, ameiagiza Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) kukamilisha ujenzi wa barabara kutoka Butiama hadi Serengeti ili kuwavitia watalii kutembelea mahali hapo.
Kuboreshwa kwa makazi hayo ni mwendelezo wa kuboresha kumbukumbu za Baba wa Taifa kwa ajili ya vizazi vya sasa na vijavyo baada ya Serikali kuwekeza katika uanzishaji wa Makumbusho ya Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere iliopo karibu na makazi hayo.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Telephone: +255282622305
Mobile:
Email: ras.mara@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.