• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

RC Mtambi kusikiliza kero za wananchi kila Jumanne

Posted on: May 23rd, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Mara Kanali Evans Alfred Mtambi leo amezungumza na watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na kuzungumzia mpango wake wa kuanza kusikiliza kero za wananchi kila siku ya jumanne kuanzia tarehe 01 Juni, 2024.

Akizungumza na watumishi hao, Mhe. Mtambi amesema atafungua kliniki maalum ya kusikiliza kero za wananchi akishirikiana na wataalamu mbalimbali waliopo katika Mkoa wa Mara.

“Huu utakuwa ni utaratibu wa kudumu kwa kila siku ya Jumanne tutasikiliza kero za wananchi ambapo wataalamu watazichakata na kila siku ya Ijumaa tutatoa mrejesho au maamuzi ya kero za wananchi waliosikilizwa wiki hiyo baada ya mimi kujiridhisha na mapendekezo yaliyotolewa na wataalamu” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amesema atahakikisha kero zote zitakazoletwa na wananchi zinasikilizwa na viongozi na watendaji wa umma katika maeneo yao ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli zao za maendeleo kwa amani.

“Tufungue milango ya ofisi za Serikali, tuwasikilize na kutatua changamoto za wananchi na kuwahudumia wananchi kwa kuzingatia maadili ya utumishi wa umma, sheria na taratibu za utumishi wa umma” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi pia amewataka Wakuu wa Wilaya, wakuu wa taasisi za umma, wenyeviti na Wakurugenzi wa Halmashauri za Mkoa wa Mara kutenga siku ya kusikiliza kero za wananchi na kutatua migogoro yao kwa kuzingatia sheria, busara na maoni ya wananchi wa eneo husika.  

Mhe. Mtambi amewataka watumishi wa Serikali kufanya kazi kwa bidii kwa kuwa wao ni wawakilishi wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye maeneo wanayotolea huduma  na kuongeza kuwa watumishi wanauwezo wa kuwafanya wananchi waipende Serikali yao au waichukie.

Wakati huo huo, Mhe. Mtambi amesikiliza kero za watumishi wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na kumtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara kufuatilia kwa ukaribu suala la kumpandisha cheo Bwana Lameck Chegeni,  Mtendaji wa Kijiji cha Kano katika Kata ya Natta.  

 Aidha, amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Serengeti kumpatia ajira ya muda Mtaalamu wa TEHAMA Bwana Mathias Ngola Samwel ambaye anajitolea katika Halmashauri hiyo kuanzia mwaka 2021.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.