• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

RC apongeza Wilaya ya Musoma uandikishaji wanafunzi

Posted on: January 18th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mohamed Mtanda leo amezungumza na Waandishi wa Habari ofisini kwake na kutoa taarifa ya uandikishaji na mapokezi ya wanafunzi wa Darasa la Awali, Darasa la Kwanza na Kidato cha Kwanza hadi kufikia tarehe 17 Januari, 2024 na ameipongeza Wilaya ya Musoma kwa kufanya vizuri katika uandikishaji.

MHe. Mtanda ameeleza kuwa taarifa zinaonyesha kuwa Wilaya ya Musoma kupitia Halmashauri zake za Halmashauri ya Wilaya ya Musoma na Manispaa ya Musoma zimefanya vizuri katika uandikishaji na mapokezi ya wanafunzi.

“Ninaipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Musoma kwa kuongoza kimkoa katika kuandikisha wanafunzi wa Darasa la Awali na kidato cha Kwanza na Manispaa ya Musoma kwa kuongoza katika kuandikisha wanafunzi wa darasa la Kwanza” amesema Mhe. Mtanda

Mkuu wa Mkoa amewataka viongozi wa Wilaya, Halmashauri, Watendaji wa Kata na Vijiji kuhakikisha wanafunzi wote waliotarajiwa kuanza masomo kwa mwaka 2024 wanapelekwa shule na wanaanza masomo.

“Nitoe wito kwa Wakuu wa Wilaya na viongozi wa ngazi zote kuhakikisha wanafanya msako wa wanafunzi wote wanaotakiwa kwenda shule wanaanza masomo kabla ya mwisho wa muda wa kupokea wanafunzi kwa mwaka 2024” amesema Mhe. Mtanda.

Mhe. Mtanda amewapongeza viongozi wote, wasimamizi wa Elimu, walimu wakuu na wakuu wa shule kwa kazi kubwa wanayoifanya na kuwataka kuhakikisha kuwa wanafunzi wote wanaotakiwa kuanza masomo wanaanza masomo bila vipingamizi.  

Taarifa iliyotolewa na Kaimu Katibu Tawala Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Bwana Bulenga Makwasa imeeleza kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Musoma imeandikisha jumla ya wanafunzi 9,212 ambapo kati yao wavulana ni 4692 na wavulana ni 4520 sawa na asilimia 96.56 ya watoto 9,540 waliotarajiwa kuandikishwa Darasa la Awali.

Halmashauri nyingine zilizofanya vizuri uandikishaji wa Darasa la Awali ni pamoja na Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti iliyoandikisha kwa asilimia 95.81 na Halmashauri ya Wilaya ya Butiama  iliyoandikisha kwa asilimia 91.99.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, Halmashauri ya Wilaya ya Musoma pia imefanya vizuri katika uandikishaji wa wanafunzi wa Kidato cha Kwanza ambapo imeandikisha wanafunzi 4,092 kati ya wanafunzi 5733 waliofaulu na kuchaguliwa kujiunga na Shule za Sekondari katika Halmashauri hiyo ambayo ni sawa na asilimia 71.

 Halmashauri nyingine zilizofanya vuzuri uandikishaji wa Kidato cha Kwanza ni Manispaa ya Musoma asilimia 69.36, Halmashauri ya Mji wa Bunda asilimia 62.13.

Aidha, taarifa hiyo imeonyesha kuwa Manispaa ya Musoma imefanikiwa kuandikisha wanafunzi 4,482 Darasa la Kwanza kati ya maoteo ya kuandikisha wanafunzi 4,437 kwa mwaka 2024 ambayo ni sawa na asilimia 101.01.   

Halmashauri nyingine zilizofanya vizuri katika uandikishaji wa Darasa la Kwanza ni Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti asilimia 99.81, Halmashauri ya Wilaya ya Rorya asilimia 96.18.

 Uandikishaji wa wanafunzi unaendelea hadi tarehe 31 March, 2024 ambapo utasitishwa hadi mwaka uandikishaji kwa ajili ya mwaka mwingine wa masomo utakapoanza.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.