Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo Mei 13, 2025 amempokea Mkuu wa Jeshi la Anga nchini Meja Jenerali Shaban Balaghashi Mani aliyeko katika Mkoa wa Mara kwa ziara ya kikazi.
Akizungumza katika mapokezi ya ugenzi huo, Mhe. Mtambi amemkaribisha sana na kumhakikishia kuwa Mkoa wa Mara upo salama na wananchi wanaendelea na shughuli zao za maendeleo na uzalishaji mali.
“Karibu sana Mkoa wa Mara, sisi tunaendelea kuchapa kazi, sisi ni mkoa wenye shughuli nyingi za uzalishaji mali, wananchi wapo wanaendelea na shughuli zao kama kawaida” amesema Mhe. Mtambi.
Mhe. Mtambi amemshukuru Meja Jenerali Mani na msafara wake kwa ushirikiano wanaoutoa katika Mkoa wa Mara na kwa kufanya ziara ili kujionea mazingira halisi ya vikosi katika maeneo mbalimbali.
Kwa upande wake, Meja Jenerali Shaban Balagashi Mani amesema kuwa yupo katika ziara ya kawaida ya kikazi katika Mikoa yote ya Kanda ya Ziwa na amemshukuru Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa mapokezi mazuri waliyoyapata.
“Ziara ya kawaiada tu ya kitendaji katika Komandi yetu huku nikikutana na changamoto za wenzetu natatua hapo hapo au kupanga mikakati ya kuitatua kwa lile jambo gumu” amesema Meja Jenerali Mani.
Katika ziara hiyo, Meja Jenerali Mani ameambatana na maafisa mbalimbali ambao wakati wa mapokezi hayo walijitambulisha kwa Mkuu wa Mkoa.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Telephone: +255282622305
Mobile:
Email: ras.mara@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.