Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mohamed Mtanda akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara, leo ameongoza mapokezi ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Gerald Musabila Kusaya ambaye amehamishiwa Mara akitokea Mkoa wa Rukwa.
Bwana Kusaya amewasili tayari kwa kuanza kutekeleza majukumu yake ambapo baada ya mapokezi amefanya kikao na Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa wa Mara na ameshiriki kikao cha Baraza la Biashara la Mkoa wa Mara.
Akizungumza katika mapokezi hayo, Bwana Kusaya amepongeza kwa mapokezi aliyoyapa na kuahidi kutoa ushirikiano kwa viongozi, watumishi, wananchi na wadau wa Mkoa wa Mara.
Bwana Kusaya anachukua nafasi ya Bwana Msalika Robart Makungu ambaye amehamishwa kwenda kuwa Katibu Tawala wa Mkoa wa Rukwa katika mabadiliko ya viongozi yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 9 Machi, 2024.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Telephone: +255282622305
Mobile:
Email: ras.mara@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.