Naibu Waziri Mkuu na Waziri wa Nishati Mhe. Dkt. Doto Mashaka Biteko anategemewa kuwaongoza waombolezaji katika mazishi ya aliyekuwa Mkurugenzi Mwendeshaji wa Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Gissima Nyamo-Hanga yatakayofanyika leo tarehe 16 Aprili, 2025 katika eneo la Mikungani, Wilaya ya Bunda.
Ratiba iliyotolewa inaonyesha kuwa ibada ya mazishi itakayoongozwa na Kanisa la KKT Bunda itaanza saa tatu kamili asubuhi, salamu za rambirambi zitatolewa kuanzia saa 4.25 hadi saa sita mchana na ibada ya mazishi itafanyika kuanzia saa sita mchana na utoaji wa heshima za mwisho utafanyika kuanzia saa saba mchana.
Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi akiambatana na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara wanatarajiwa kushiriki mazishi haya.
Mhandisi Nyamohanga na dereva wake walifariki katika ajali iliyotokea usiku wa kuamkia tarehe 13 Aprili, 2025 katika Kata ya Nyatwali, jirani na geti kuu la Hifadhi ya Taifa ya Serengeti lililopo eneo la Ndabaka, Wilaya ya Bunda.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Telephone: +255282622305
Mobile:
Email: ras.mara@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.