• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI aanza ziara Bunda

Posted on: June 8th, 2023

Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Wilson Charles Mahera ameanza ziara yake ya siku tatu katika Mkoa wa Mara tarehe 3 Juni, 2023  kwa kutembelea Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda,  Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bunda na Hospitali ya Manyamanyama iliyopo katika Mji wa Bunda.

Akizungumza katika ukaguzi na vikao na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na Halmashauri ya Mji wa Bunda, Dkt. Mahera amemuagiza Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kuwasilisha ofisini kwake taarifa ya Ukaguzi wa Ndani kuhusiana na ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

“Ninatoa wiki mbili taarifa ya ukaguzi wa ndani ya hospitali hii ifike mezani kwangu ili kujiridhisha kuhusu matumizi ya fedha za ujenzi  wa hospitali hii  na hususan zilizoletwa katika awamu ya kwanza ya ujenzi huu” alisema Dkt. Mahera.

Dkt. Mahera ameeleza kuwa taarifa ya ukaguzi  wa ujenzi wa hospitali hiyo itatoa mwanga kwa yaliyokuwa yamejiri wakati wa ujenzi ili kama kulikuwa na ubadhilifu au ukiukaji wa maadili ya utumishi wa umma wahusika waweze kufuatiliwa na Serikali.

Aidha, Dkt. Mahera amemuagiza Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda kuendelea kufuatilia kwa ukaribu kesi ya wizi wa vifaa vya hospitali iliyopo Polisi ili wahusika waweze kuchukuliwa hatua ikiwa ni pamoja na kurejesha vifaa hivyo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi milioni 56.

Dkt. Mahera amemtaka Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kufanya usimamizi wa karibu zaidi katika ujenzi wa hospitali hiyo ili kurekebisha mapungufu mbalimbali yaliyojitokeza katika usimamizi wa ujenzi wa hospitali hiyo.  

Naibu Katibu Mkuu TAMISEMI ameagiza pia kufufuliwa kwa kamati za ujenzi wa hospitali hiyo kulingana na mwongozo wa force account ili kuendelea kusimamia mradi huo kama ilivyokuwa awali kabla hazijaacha kufanyakazi ya usimamizi. 

Wakati huo huo, Dkt. Mahera na timu aliyoambatana nayo wamepongeza ubora wa majengo yaliyojengwa katika Hospitali ya Wilaya ya Bunda pamoja na ujazaji wa taarifa za masuala ya chanjo katika hospitali hiyo.

Wakati huo huo, Dkt. Mahera amewataka Waganga Wakuu wa Halmashauri kuhakikisha wanafunga mfumo wa kukusanyia mapato katika vituo vya kutolea huduma za afya wa GOTHOMIS katika vituo vyote vya Serikali ili kudhibiti upotevu wa mapato katika vituo hiyo.  

“Kila kituo cha kutolea huduma za afya kiwe na angalau kompyuta sita na kifungwe mfumo wa GOtHOMIS ifikapo tarehe 30 Juni, 2023 ili kudhibiti upotevu wa mapato ya Halmashauri” amesema Dkt. Mahera.

Katika Hospitali ya Mji wa Bunda Dkt. Mahera ameipongeza Halmashauri hiyo kwa ujenzi wa majengo matatu yaliyo katika hatua mbalimbali na kuitaka Halmashauri kufuata mwongozo wa force account katika utekelezaji wa ujenzi huo.

Katika Hospitali ya Manyamanyama Dkt. Mahera amezungumza na timu ya wataalamu kutoka Wizara ya Afya inayofanya ukaguzi na uwajengea uwezo watumishi katika hospitali hiyo ili kupata mrejesho wa mambo waliyoyabaini katika uwepo wao katika Mkoa wa Mara katika kipindi cha wiki tatu walizokaa katika Hospitali hiyo na Kituo cha Afya Nyasho kilichopo katika Manispaa ya Musoma.

Ratiba ya viongozi hao inaonyesha kuwa tarehe 4 Juni, 2023 Dkt. Mahera anaendelea na ziara yake kukagua miundombinu ya afya inayojengwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Halmashauri ya Mji wa Tarime na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.

Katika ziara hiyo, Dkt. Mahera aliongozana na wataalamu wengine wanne kutoka Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Dkt. Zabron Masatu, Katibu Tawala wa Wilaya ya Bunda, watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na Halmashauri za Mji wa Bunda na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.