• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Mwenge wa Uhuru waanza mbio zake katika Mkoa wa Mara

Posted on: July 4th, 2023

Mwenge wa Uhuru leo umeanza kukimbizwa katika Mkoa wa Mara kwa kukimbizwa katika Wilaya ya Serengeti ambapo umezindua miradi miwili, kuweka mawe ya misingi katika miradi mitatu, kutembelea kikundi cha vijana cha ufugaji wa kondoo na vilabu vya wapinga rushwa na mazingira.

Miradi iliyozinduliwa ni pamoja na mradi wa daraja la Tabora B linalosimamiwa na Mamlaka ya Hifadhi za Taifa (TANAPA) ikiwa ni sehemu ya madaraja matano na mradi wa vyumba vya madarasa viwili, ofisi ya walimu, tenki la maji na vyoo vya wanafunzi katika Shule ya Msingi Kisangula miradi ambayo ni sehemu ya miradi mikubwa inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) katika Wilaya ya Serengeti.

Aidha, Mwenge wa Uhuru umeweka mawe ya msingi katika mradi wa maji unaosimamiwa na Wakala wa Maji Mijini na Vijijini (TARURA) katika Kijiji cha Nyibirekera na mradi wa zahanati katika Kijiji cha Nyibirekera  ikiwa ni sehemu ya miradi ya ujenzi wa zahanati, nyumba za watumishi na miundombinu ya afya inayofadhiliwa na Benki ya Maendeleo ya Ujerumani (KFW) na mradi wa ujenzi wa Chuo cha Ufundi cha World Changer kinachofadhiliwa na Taasisi moja ya kidini nchini Ujerumani.

Mbali na miradi hii, Mwenge pia umetembelea kikundi cha vijana wanaofuga kondoo na kilichopata mkopo wa Halmashauri katika eneo la Natta na vilabu vya Rushwa na Mazingira katika Shule ya Msingi ya Kisangula.

Akizungumza kuhusiana na miradi ya Wilaya ya Serengeti, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Mhe. Abdalla Shaib Kaim ameeleza kuwa Mwenge wa Uhuru umekagua na kuridhishwa na nyaraka za miradi, ubora na gharama za miradi ya Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.

Mhe. Kaim ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti kuwasaidia vijana wanaojihusisha na kikundi cha ufugaji wa kondoo ili kuweza kukua na kufanya uzalishaji ambao utaongeza kipato na ajira kwa wanakikundi na wananchi wengine katika eneo hilo.

Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Wilaya ya Serengeti zilihudhuriwa pia na Mkuu wa Wilaya ya Serengeti, Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Serengeti, Mbunge wa Serengeti, viongozi na watendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na wananchi wa Wilaya ya Serengeti.

Kesho tarehe 5 Julai, 2023 Mwenge wa Uhuru utaendelea na mbio zake katika Halmashauri ya Wilaya ya Butiama ambapo ukiwa hapo unategemewa kuwasha Mwenge wa Mwitongo.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.