• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Mtanda Ashiriki ujenzi wa Sekondari ya Wasichana Mkoa wa Mara

Posted on: September 22nd, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mohamed Mtanda leo tarehe 19 Septemba, 2023 ameendelea na ziara yake katika Wilaya ya Bunda ambapo amekagua na kushiriki ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Mara inayojengwa katika eneo la Bulamba, Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Katika ziara hiyo, Mhe. Mtanda ameshiriki kuchimba kifusi na kujaza kifusi katika baadhi ya majengo yanayoendelea kujengwa katika eneo hilo na kumwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri na Ofisi ya Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Miundombinu Mkoa wa Mara kufuatilia kwa ukaribu ujenzi wa shule hiyo.

“Wenzetu mikoa mingine shule hizi zimekamilika lakini kutokana na changamoto zilizokuwepo bado ujenzi wa shule hii unaendelea, niwaombe tuongeze kasi ya ujenzi wa shule hii” amesema Mhe. Mtanda.

Aidha, Mhe. Mtanda amemwagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kumchukulia hatua mtumishi wa kitengo cha manunuzi ambaye hakuonekana ofisini kwa muda wa miezi mitatu bila kupewa ruhusa na mwajiri.

Mhe. Mtanda amewaagiza Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kusimamia utekelezaji wa miradi ili kuikamilisha kwa kutumia fedha zinazoletwa na Serikali badala ya kutafuta nyongeza au kutumia fedha za mapato ya ndani katika miradi hiyo.

Mheshimiwa Mtanda pia amewataka Maafisa Elimu wa Halmashauri na Waganga Wakuu wa Halmashauri kufuatilia kwaukaribu miradi ya sekta zao inapokuwa inatekelezwa.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa alitembelea mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mji wa Bunda na Sekondari ya Bunda Stoo  katika Halmashauri ya Mji wa Bunda na Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Mara, Shule ya Sekondari Sunsi, Shule ya Sekondari  kasuguti zilizopo Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

 Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa aliambatana na Mkuu wa Wilaya ya Bunda na Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Bunda, Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Afya, wawakilishi wa Makatibu Tawala Wasaidizi sehemu za Elimu na Miundombinu, wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa taasisi za umma,  baadhi ya watumishi wa Halmashauri.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.