Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mohamed Mtanda leo ofisini kwake amewaapisha wajumbe wa Baraza la Ardhi na Nyumba Wilaya ya Musoma.
Akizungumza wakati akiwaapisha wajumbe hao, Mhe. Mtanda amewataka wajumbe wa baraza hilo kuzingatia haki na kujiepusha na masuala ya rushwa kwani kwa kufanya hivyo watakuwa wanawakwamisha wananchi kupata haki na kwenda kinyume na matakwa ya Baraza la Nyumba na Ardhi.
Aidha, Mhe. Mtanda amemtaka Mwenyekiti wa Baraza la Ardhi na Nyumba kuwajengea uwezo wajumbe walioapishwa kuhusu masuala ya ardhi na namna ya kutekeleza majukumu yao kama wajumbe wa baraza hilo.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Telephone: +255282622305
Mobile:
Email: ras.mara@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.