• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

MTANDA akabidhi magari ya usimamizi wa sekta ya afya

Posted on: February 10th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mohamed Mtanda leo amekabidhi magari matano ya usimamizi wa Sekta ya Afya na kuwataka viongozi na wasimamizi wa sekta ya afya kuhakikisha magari hayo yanatumika kwa malengo yaliyokusudiwa.

Akizungumza wakati wa kukabidhi magari hayo, Mhe. Mtanda amewataka viongozi na watendaji wa Mkoa na Halmashauri kuhakikisha magari hayo yanatunzwa kwa mujibu wa taratibu za Serikali na yanatumika kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuboresha huduma za sekta ya afya Mkoa wa Mara.

“Sitarajii kuona magari haya yakitumika kubeba mizigo mizito na mikaa, haya ni magari ya usimamizi na yatumike kufanya shughuli za usimamizi katika sekta ya afya” amesema Mhe. Mtanda.

Mhe. Mtanda pia amewataka wasimamizi wa magari hayo kuangalia mienendo ya madereva wao ili kujiridhisha na uendeshaji salama wa magari ya Serikali kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma.

Aidha, Mhe. Mtanda amewakumbusha viongozi kuhusu maelekezo aliyoyatoa awali kuhusu utengenezaji wa magari ya Serikali ili yaweze kutoa huduma zilizokusudiwa.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Dkt. Zabron Masatu ameeleza kuwa magari hayo matano yanayokabidhiwa ni sehemu ya magari 33 ya  sekta ya afya yaliyotolewa na Serikali kwa Mkoa wa Mara katika mwaka huu wa fedha.

“Kwa sasa tunasubiri magari ya usimamizi ya Halmashauri tano ambayo bado hayajapokelewa na yanatarajiwa kupokelewa wakati wowote kuanzia sasa” amesema Dkt. Masatu.

Dkt. Masatu ameeleza kuwa tayari baadhi ya magari ikiwa ni pamoja na magari ya kubeba wagonjwa  kwa ajili ya Halmashauri zote za Mkoa wa Mara na Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere yamepokelewa na kukabidhiwa kwa walengwa.   

Halmashauri zilizokabidhiwa magari ya usimamizi wa sekta ya afya leo ni Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Halmashauri ya Wilaya ya Rorya, Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti na Halmashauri ya Wilaya ya Butiama.

Dkt. Masatu ameeleza kuwa magari hayo yataboresha ukaguzi na usimamizi wa vituo vya kutolea huduma za afya na kuwawezesha wasimamizi wa sekta ya afya ngazi za Halmashauri na Mkoa kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.   

Magari 33 yametolewa na Serikali kwa ajili ya Usimamizi wa sekta ya Afya magari 13, kwa ajili ya Mkoa, Halmashauri, Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere, Chuo cha Maafisa Tabibu Musoma na magari ya kubeba wagonjwa 20 kwa ajili ya Halmashauri tisa na Hospitali ya Rufaa ya Kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere (Kwangwa).

 Hafla ya kukabidhi magari imehudhuriwa pia na Katibu wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, Wakuu wa Wilaya, Makatibu Tawala Wasaidizi na Wakuu wa Vitengo vya Sekretarieti ya Mkoa wa Mara, Wakurugenzi wa Halmashauri na baadhi ya watendaji wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na Halmashauri.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • RC atoa siku 14 wanafunzi wote Sekondari ya J. K. Nyerere wapate chakula shuleni

    July 28, 2025
  • Kusaya apokea ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama

    July 25, 2025
  • Mtambi ataka matumizi ya GOTHOMIS kwa asilimia 100 Mara

    July 25, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.