• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Mtambi afanya ziara Bunda

Posted on: June 27th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 26 Juni, 2024 amefanya ziara kwa mara ya kwanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Bunda ambapo akiwa katika Halmashauri hiyo amekagua miradi ya maendeleo, kuzungumza na watumishi na kushiriki kikao cha Baraza cha kujibu hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

Mhe. Mtambi ameanza ziara yake kwa kutembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa shule ya Sekondari ya Wasichana ya Mkoa wa Mara inayojengwa katika Halmashauri hiyo na kumwagiza Mkuu wa Wilaya kuhamia kwa muda katika shule hiyo inayotarajiwa kuanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano kuanzia tarehe 30 Juni, 2024.

“Ninataka uhamie hapa ili kusimamia usafi wa mazingira, marekebisho ya baadhi ya maeneo niliyoagiza na ukamilishaji wa utengenezaji wa samani kwa ajili ya wanafunzi” amesema Mhe. Mtambi na kuitaka Halmashauri hiyo kuyafanyia kazi maagizo yake aliyoyatoa.  

Baada ya hapo, Mhe. Mtambi ametembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa nyumba ya Mkurugenzi wa Halmashauri na nyumba ya wakuu wa idara zinazoendelea kujengwa katika eneo la Mumagunga, Kibara na kuagiza Halmashauri kukamilisha mradi huo haraka ili Mkurugenzi aweze kuhamia.    

Akiwa kwenye mradi huo, Mkuu wa Mkoa amepongeza ubora wa ujenzi wa mradi huo ambao umefikia asilimia 95 ya utekelezaji  na kutoa muda wa miezi miwili Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo awe amehamia na kuleta taarifa ofisini kwake za utekelezaji wa agizo hilo.    

Aidha, Mkuu wa Mkoa pia amekagua maendeleo ya ujenzi wa jengo la ofisi ya Halmashauri ya Wilaya ya Bunda na kumtaka mkandarasi wa mradi huo Suma JKT kukamilisha mradi huo kwa haraka.

Kanali Mtambi ameitaka Halmashauri ya Wilaya ya Bunda kusafisha mazingira kuzunguka mradi huo na kuandaa upatikanaji wa mahitaji ya ujenzi ili kumrahisishia mkandarasi wa mradi huo kutekeleza mradi  kwa wakati.

Akiwa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda pia Mhe. Mtambi amezungumza na wafanyakazi wa Halmashauri hiyo na kuwakumbusha kufanyakazi kwa bidii na weredi na kuongeza ubunifu ili kuwatumikia kwa ufanisi wananchi.

Mkuu wa Mkoa amehitimisha ziara yake kwa kuhudhuria kikao maalum cha Baraza la Madiwani kwa ajili ya kujadili hoja za CAG  vikao vilivyofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Katika ziara hiyo, Mkuu wa Mkoa aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa, Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Bunda, Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Bunda, maafisa kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Mara na Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • RC atoa siku 14 wanafunzi wote Sekondari ya J. K. Nyerere wapate chakula shuleni

    July 28, 2025
  • Kusaya apokea ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama

    July 25, 2025
  • Mtambi ataka matumizi ya GOTHOMIS kwa asilimia 100 Mara

    July 25, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.