• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Mkoa wa Mara wadhamiria kuboresha Elimu

Posted on: February 25th, 2020

Mkoa wa Mara umedhamiria kuboresha elimu ya Msingi na Sekondari mkoani humu kwa vitendo kwa kuboresha mazingira ya kujifunzia na ufundishaji na kuvunja kabisa mtandao wa wizi wa mtihani uliokuwepo miaka ya nyuma.

Akizungumza kwenye Kongamano la Wadau wa Elimu wa Mkoa wa Mara lililofanyika tarehe 23 Februari 2020, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Adam Malima amesema tumejitahidi sana kuboresha miundombinu ya shule za msingi na sekondari.

Akizungumzia kuhusu mtandao wa wizi wa mitihani mkoani Mara, Mheshimiwa Malima alisema “Mkoa wa Mara ulikuwa ni kitovu cha wizi wa mitihani hapa nchini, lakini tumefanikiwa kuuvunja mtandao wa wizi wa mitihani na sasa tunachokipata ndio hali halisi”. Amesema japokuwa awali Mkoa ulionyesha unafaulisha sana, lakini baadaye waligundua ufaulu huo ulitokana na wizi wa mtihani.

Mheshimiwa Malima amesema, wizi huu wa mitihani ungeachwa uendelee ungejenga kizazi cha watu wengi sana ambao hawajui chochote lakini wanavyeti vizuri.  “Ingekuwa ni hatari kwa maendeleo ya taifa letu kwa siku za baadaye”. Amesema katika mtandao huo kulikuwa na uhusika wa wadau karibu wote wa elimu na hususan wazazi ambao walikuwa wanatoa fedha za kununua mitihani.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa mdahalo huo na Mbunge wa Musoma Vijijini  Prof. Sospeter Muhongo alisema zamani Mkoa wa Mara ulikuwa na shule mbili tu za sekondari za umma Mara Sekondari na Musoma Alliance lakini zilikuwa zinafanya vizuri sana na wengi waliohitimu hapo walifaulu na kufanya vizuri sehemu nyingine walizoenda kusoma.

“Enzi zetu sekondari za binafsi zilizokuwepo chache lakini zilikuwa hazitushindi kabisa tuliokuwa tunasoma shule za serikali katika mashindano ya kitaaluma, zilitushinda katika mambo mengine”. Alisema Mhe. Muhongo. Alisema sababu kubwa zilizochangia wao kufanya vizuri ilikuwa ni ubora wa walimu waliokuwa wanawafundisha na mazingira mazuri ya kusomea katika maeneo ya shule yaliyokuwepo wakati huo.

Kongamano hilo lililofanyika katika Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Songe, lilihudhuriwa pia na wazazi, wanafunzi wa shule za msingi na sekondari, walimu, maafisa elimu wa ngazi za kata, halmashauri na ngazi ya mkoa. Aidha walihudhuria vyama mbalimbali ikiwemo Chama cha Walimu, Vyama vya Wakuu wa Shule, Vyama vya walimu wakuu, wanasiasa, watu maarufu na wananchi wakawaida.

Kongamano lilifanikiwa kutoa maazimio tisa ambayo ni pamoja na halmshauri ziandae mikakati ya kuboresha miundombinu ya elimu shuleni; mwanafunzi ambaye hataonekana shuleni kwa siku saba mfulilizo atalazimika kufika shuleni na mzazi wake na utaratibu wa utoaji chakula kwa wanafunzi shuleni ni lazima hivyo wazazi ambao hawatachangia chakula watachukuliwa hatua za kisheria.

Pia kongamano lilikubaliana kuwa walimu watoro wafikishwe kwenye mamlaka ya nidhamu na maamuzi yatolewe haraka ili kuimarisha uwajibikaji wa walimu; mahusiano kati ya walimu na jamii yaimarishwe ili kuboresha ufundishaji na ujifunzaji; vitendo vya mimba kwa wanafunzi na ukatili kwa watoto wa kike vitengenezewe mkakati wa kuvitokomeza na uwepo wa mpango bora wa kuishirikisha jamii kwenye maendeleo ya shule.

Aidha kongamali liliazimia kuwa serikali za vijiji ziwe na mkakati wa kuhakikisha usalama wa walimu kwenye mazingira yao na kongamano lingine la kutathmini maazimio ya kongamano hili lifanyike tarehe 30 Agosti, 2020.  

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.