Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mohamed Mtanda leo tarehe 26 Mei, 2023 ameshiriki msiba wa Mhe. Herman Kiligini, Mbunge wa Musoma Vijijini na Waziri wa Kilimo na Mifugo mstaafu uliopo katika eneo la Kamnyonge, Manispaa ya Musoma.
Akiwa msibani hapo, Mhe. Mtanda amesaini kitabu cha maombolezo na kutoa pole kwa wafiwa wote wanaohusika na msiba huo.
Mhe. Kiligini alifariki tarehe 24 Mei, 2023 katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara na anatarajiwa kusafirishwa leo kwenda katika Kijiji cha Muryaza, Wilaya ya Butiama kwa ajili ya mazishi yatakayofanyika tarehe 27 Mei, 2023.
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Telephone: +255282622305
Mobile:
Email: ras.mara@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.