• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Mhe. Mtanda aanza kazi Mara

Posted on: May 26th, 2023

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mohammed Mtanda leo tarehe 25 Mei, 2023 amewasili Mkoani Mara na kukabidhiwa rasmi ofisi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee katika hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Uwekezaji, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Awali, viongozi mbalimbali wakiwemo Wakuu wa Wilaya za Mkoa wa Mara, Kamati ya Usalama ya Mkoa, Makatibu Tawala wa Wilaya,  wamempokea Mheshimiwa Mtanda katika eneo la Ndabaka, Wilaya ya Bunda.

Baada ya mapokezi, Mhe. Mkuu wa Mkoa amefika katika Ofisi za Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara kwa ajili ya kutia saini kitabu cha wageni na kujitambulisha na kuzungumza na viongozi wa Chama cha Mapinduzi.

Msafara wa Mkuu wa Mkoa ulielekea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ambapo alipokelewa na viongozi wa taasisi za Umma, Wakuu wa Idara na Vitengo, watumishi  wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na viongozi wa CCM Mkoa wa Mara.

Hafla fupi ya makabidhiano ilifanyika katika Ukumbi wa Uwekezaji uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara ambapo aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Meja Jenerali Suleiman Mungiya Mzee alimkabidhi ofisi.

Akizungumza baada ya kukabidhiwa ofisi, Mheshimiwa Mtanda amewataka  viongozi na watumishi wote kushirikiana na kufanyakazi kwa ubunifu, uadilifu na uaminifu ili kuwahudumia wananchi wa Mkoa wa Mara kwa ufanisi.

“Sisi sote tuna wajibu wa kutekeleza ili kuwaletea maendeleo wananchi wa Mkoa wa Mara na ndio maana tupo hapa katika Mkoa huu, tutimize wajibu wetu” alisema Mheshimiwa Mtanda.

Aidha, ametumia nafasi hiyo Kumshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kumteua kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Mhe. Mtanda amehitimisha siku kwa kushiriki katika Kikao cha Kamati ya Siasa ya Manispaa ya Musoma na Viongozi wa Mitaa na Kata za Manispaa ya Musoma.

Mhe. Mtanda aliteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan tarehe 23 Mei, 2023 na kuapishwa rasmi tarehe 24 Mei, 2023.    

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.