• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Mgodi wa Dhahabu wa North Mara watozwa faini

Posted on: April 26th, 2022

Serikali imeutaka Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara kulipa faini ya shilingi bilioni moja ndani ya siku 14 baada ya bomba lake la maji machafu   kuachia na kutiririsha maji machafu karibu na makazi ya watu katika eneo la Nyamongo, Wilaya ya Tarime.

Akisoma faini hiyo, Mkurugenzi Mkuu wa Baraza la Usimamizi wa Mazingira (NEMC) Dkt. Samuel G. Mafwenga, amesema kuwa faini hiyo ni kwa mujibu wa kifungu cha 187 cha Sheria ya Usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004.

“Faini hii isaidie kuikumbusha migodi yote hapa nchini wajibu wao wa kulinda mazingira na kuhakikisha kwamba jambo kama hili halitajirudia tena wakati mwingine” alisema Dkt. Mafwenga.

Dkt. Mafwenga ameeleza kuwa japokuwa maji machafu hayo yalikuwa hayana sumu kama ilivyotaarifiwa awali, lakini maji hayo sio salama kwa ajili ya matumizi ya kawaida ya binadamu.

Akizungumza baada ya kukagua na kupata maelezo ya eneo hilo, Waziri wa Madini Mheshimiwa Dotto Biteko ameutaka mgodi huo kuimarisha mahusiano baina yake na wananchi wa eneo la Nyamongo ulipo mgodi huo.

“Malalamiko mengi yaliyopo hapa leo yanatokana na mahusiano mabovu yaliyokuwepo kati ya mgodi na wananchi wa Nyamongo. Mahusiano na wananchi yakiwa mazuri yatakuwa na faida kwa Mgodi na wananchi wanaouzunguka mgodi huu” amesema Mheshimiwa Biteko.

Mheshimiwa Biteko ameeleza kuwa suala la bomba la maji machafu kupasuka na kutiririsha maji muda mrefu bila uongozi wa mgodi kujua limetokana na  uzembe na sio bahati mbaya.

“Leo akiingia mwananchi katika eneo la mgodi na kujaribu kuiba ndani ya nusu saa atakuwa ameshakamatwa, lakini bomba la maji machafu linaachia na kutiririsha maji machafu kwa masaa zaidi ya manne bila Menejimenti  ya Mgodi kujua ni uzembe” alisema Mheshimiwa Biteko.

Mheshimiwa Biteko pia ameagiza kuondolewa mara moja kwa Afisa Mgodi  Mkazi ambaye alikuwa ni mwakilishi wa Wizara ya Madini katika Mgodi wa Dhahabu wa North Mara kutokana na uzembe huo.

Kuhusu malipo ya fidia ya maeneo ambapo mgodi unataka kuyachukua,  Mheshimiwa Biteko ameeleza kuwa wananchi wa Nyamongo wanatumiwa na watu wachache wenye nia ovu kusitisha zoezi la tathmini na hivyo kwa sasa hawawezi kulipwa fidia mpaka tathmini ikamilike.

Mheshimiwa Biteko ameeleza kuwa fedha za Uwajibikaji kwa Jamii (CSR) shilingi bilioni 5 zinazotolewa na mgodi huo zitekeleze miradi ya maendeleo kwa wananchi.

“Mimi ninakuomba Mkuu wa Mkoa, hili jambo ndani ya wiki mbili liishe na miradi ya maendeleo ya wananchi ianze kutekelezwa, watu wa Nyangongo wanaulaumu mgodi kumbe mgodi ulishatoa fedha hizo” alisema Mheshimiwa Biteko.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Ally Salum Hapi ameeleza kuwa miradi iliyotekelezwa kwa fedha za Uwajibikaji kwa Umma (CSR) kupitia Kamati ya Maendeleo ya Jamii (CDC) zilikuwa zinatumika vibaya kutekeleza miradi ndio maana Kamati hiyo ameivunja rasmi.

Mheshimiwa Hapi ameeleza kuwa miradi hiyo itaanza kutekelezwa mara baada ya miradi hiyo kuwa imepitishwa na mamlaka za Serikali ambao ndio itawajibika kama utekelezaji ukiwa mbaya.

“Tunataka miradi yenu ikamilike kwa wakati, wananchi msitumike kama kichaka kwa watu kuchukua fedha za miradi ya maendeleo kwa manufaa yao binafsi” alisema Mheshimiwa Hapi.

Mkuu wa Mkoa ameeleza kuwa uongozi wa Mkoa umejipanga vizuri na ndani ya muda mfupi ujao miradi iliyokuwa imependekezwa itaanza kutekelezwa chini ya usimamizi wa Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Tarime.

Bomba la maji machafu yanayotoka kwenye miamba liliachia kwenye maungio yake yakiwa yanaenda kwenye bwawa la kuyasafisha tarehe 23 Aprili 2022 katika eneo la Nyamwaga na kuzua taharuki kuwa maji hayo yalikuwa yana sumu.

Hata hivyo Mamlaka za Serikali zimethibitisha kuwa maji hayo ni machafu lakini hayana sumu kama ilivyokuwa imedhaniwa hapo awali na kuzua taharuki miungoni mwa wananchi.  

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.