• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Masatu afungua kikao cha Tathini ya Elimu Mara

Posted on: June 3rd, 2024

Kaimu Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Dkt. Zabron Masatu, leo amefungua kikao cha tathmini ya utekelezaji wa kazi kwa Wasimamizi wa Elimu Mkoa wa Mara na kuwapongeza kwa kubuni kikao hicho cha kujadili utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Sekta ya Elimu kwa kila robo mwaka.

Akizungumza katika kikao hicho Dkt. Masatu amewataka wasimamizi hao kufanya vikao kama hivyo katika ngazi za Halmashauri na shule zilizopo ili kuboresha elimu katika Mkoa wa Mara.

“Ninaipongeza sana Sehemu ya Elimu kwa kuanzisha vikao vya tathmini ambavyo vinafanyika katika kila robo kwa ngazi ya Mkoa ni jambo zuri na la kuigwa kwa Sehemu na Vitengo vingine katika utekelezjai wa majukumu yao” amesema Dkt. Masatu.

Dkt. Masatu amepongeza kikao hicho kujadili suala la utoaji wa chakula mashuleni ambalo amesema kuwa ni muhimu sana katika utekelezaji wa Mwongozo wa Kitaifa wa utoaji wa Chakula masuleni na mkataba wa lishe wa Kitaifa.

Dkt. Masatu ametaka kuwepo na mipango thabiti ya utekelezaji na usimamizi wa shughuli za elimu na  kuzihusisha sekta nyingine pale inapohitajika.

Kwa upande wake, Kaimu Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Elimu Bwana Bulenga Makwasa ameeleza kuwa Sehemu ya Elimu imeanzisha utaratibu wa kufanya vikao vya tathmini katika kila robo mwaka ili kuinua ubora wa elimu na kuondoa  baadhi ya changamoto zilizokuwa zinakwamisha maendeleo ya elimu.

“Kuanzia  mwaka huu wa fedha wa 2023/2024 tumeanza kufanya tathmini hizi ambazo zinawahusisha Maafisa Elimu wote wa Halmashauri pamoja na wasaidizi wao ili kujadili masuala mbalimbali yanayohusu maendeleo ya elimu katika Mkoa wa Mara” amesema Bwana Makwasa.  

Bwana Makwasa amesema katika kikao hicho mambo mbalimbali yatajadiliwa ikiwemo taarifa ya tathmini ya utekelezaji wa KPI katika robo ya pili ya mwaka 2024 ya kila Halmashauri itakayowasilishwa na Maafisa Elimu wa Halmashauri.

Bwana Makwasa amesema jambo linguine litakalojadiliwa ni taarifa ya maandalizi ya Wiki ya Elimu ya Watu Wazima, 2024 ambapo Maafisa Elimu wa Halmashauri watawasilisha maandalizi ya kila Halmashauri.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.