• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Mara yaweka Mikakati ya UVIKO 19

Posted on: July 19th, 2021

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Albert Gabriel Msovela amewataka wasimamizi wa huduma za Afya katika Mkoa wa Mara kutengeneza na kuja na  mkakati madhubuti wa namna bora ya kuendelea kupambana na maambikizi ya  uviko 19 katika Mkoa wa Mara.

Bwana Msovela ametoa kauli hiyo leo tarehe 16 Julai 2021 wakati wa kikao cha Timu ya Usimamizi wa Huduma za afya ngazi ya Mkoa na Halmashauri kilichofanyika katika ukumbi wa Chuo cha Waganga Musoma (COTC) ili kujadili na kuweka mikakati ya kukabiliana na Uviko 19.

"Tunapotoka hapa kama wataalamu tunaohusika na masuala ya Afya ndani ya Mkoa inabidi tutengeneze mapendekezo na maazimio juu ya namna ya kupambana na Uviko 19 ili itusaidie katika kuona namna gani Mkoa unaweza kupunguza maambukizi” alisema Bwana Msovela  na kuwataka waendelee kutoa huduma huku wakizingatia njia za kujikinga na maambukizi kwa sababu Watumishi wakichukua tahadhari hata wananchi wengine wataiga kutoka kwao maana mabadiliko yoyote yanaanza na watendaji kabla ya kufika kwa wananchi.

"Wataalamu tunapotoa huduma tuzingatie njia za kutumia katika kujiepusha  na janga la Corona kwa kuvaa barakoa, kunawa mikono mara kwa mara kwa maji tiririka na sabuni, kukaa umbali unaohitajika na kuepuka misongamano isiyo ya lazima.

Aidha amewataka  wananchi kuendelea kuchukua tahadhari kuhusu kujikinga na janga la Corona kwa kuendelea kufuata ushauri na elimu inayotolewa na wataalamu wa Afya ikiwemo kuepuka misongamano isiyo ya lazima, kunawa mikono kwa kutumia maji tiririka, kutumia vitakasa mikono na kuvaa barakoa.

Katika hatua nyingine Katibu Tawala amewataka Watumishi wa sekta ya Afya kufanya kazi kwa upendo, ushirikiano na kuthaminiana kila mmoja katika nafasi yake ili katika utekelezaji wa majukumu kuwepo na mnyororo wa uelewa kuanzia ngazi ya juu hadi chini.

Aidha, amewataka Waganga Wakuu wa Halmashauri kuhakikisha katika kila kituo Cha kutolea huduma za Afya kunafungwa mfumo wa kielektroniki wa ukusanyaji wa mapato (GOTHOMIS) ili kuepusha mianya ya wizi na upotevu wa mapato ya serikali.

Awali akimkaribisha Katibu Tawala, Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Frolian Tinuga amesema kuwa wagonjwa wa Corona katika Mkoa wa Mara wapo na jitihada za kuendelea kutoa elimu kwa wananchi juu ya namna ya kukabiliana na maambukizi zinafanyika hivyo kikao hiki kina lengo la kuweka mapendekezo na maazimio ya namna bora ya kuboresha zaidi mfumo na njia za kupambana na maambukizi kwa wananchi.

"Hakuna njia mpya za kujikinga na Uviko 19 zaidi ya zile zilizopo lakini kukutana kwetu inabidi tuweke maazimio na mikakati itakayoboresha na kutuwezesha kukabiliana na maambukizi kwa kuwafikia wananchi wote na kuwapatia elimu ya namna ya kupambana na ugonjwa huu.

Sambamba na hilo Dkt. Frolian amewaagiza wasimamizi wa huduma za Afya ngazi ya Halmashauri kuendelea kutoa Elimu kwa wananchi kuhusu kujikinga na Uviko 19 kwa kutembelea maeneo yenye mikusanyiko kutumia radio, magari ya matangazo pamoja na kuhakikisha  katika vituo vyote vya kutokea huduma za Afya kunakuwepo njia zote za kujikinga na maambukizi ikiwemo uwepo wa  maji ya kunawa na sabuni,vitakasa mikono pamoja na kusisitiza wahudumu wote na wananchi kuvaa barakoa pindi watoapo na kupata huduma.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.