• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

MARA yawaomba waandishi kuelimisha jamii

Posted on: December 19th, 2023

Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Afya, Lishe na Ustawi wa Jamii Dkt. Zabron Masatu leo Desemba 11, 2023 amefungua mafunzo ya Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mara yanayofadhiliwa na Mradi wa Afya Thabiti unaotekelezwa na Shirika la AMREF Afrika na kuwataka Waandishi wa Habari kutoa elimu za mapambano dhidi ya UKIMWI.

Akizungumza wakati wa uhufunguzi wa mafunzo hayo yaliyofanyika katika Ukumbi wa Mwembeni Complex, Dkt Masatu ameeleza kuwa Waandishi wa Habari wanaomchango mkubwa sana katika kuielimisha jamii katika mapambano hayo.   

“Jamii ikujua umuhimu wa kupima afya na ikapima na kupokea majibu na ushauri wa wataalamu  inaweza kusaidia katika kupunguza maambukizi ya UKIMWI” amesema Dkt. Masatu

Dkt. Masatu ameeleza kuwa ili kufanikiwa kupunguza kasi ya maambukizi katika Mkoa wa Mara, ushirikiano baina ya Serikali, watoa huduma za afya na Waandishi wa Habari unahitajika sana ili kuweze kufikia malengo ya kupunguza maambukizi.

Aidha, Dkt. Masatu amewashukuru sana Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Mara kwa ushirikiano wanaoutoa katika kutangaza shughuli, Kampeni na miradi mbalimbali ya Sekta ya Afya.

“Dunia inalenga kuwa ifikapo mwaka 2030 kusiwepo maambukizi ya UKIMWI na hili litafanikiwa kama Waandishi wa Habari na vyombo vya Habari vitashiriki katika kuuelimisha umma kuhusu namna ya kujiepusha na maambukizi ya UKIMWI” amesema Dkt. Masatu.

Kwa upande wake Mratibu wa Upimaji UKIMWI na Tohara Kinga Mkoa wa Mara Bwana Felix Mtaki  ameeleza kuwa kiwango cha maambukizi katika Mkoa wa Mara kimepanda kutoka asilimia 3.6 miaka mitano iliyopita hadi asilimia 5 mwaka jana.

Bwana Mtaki ameeleza kuwa maambukizi hayo yameongezeka kutokana na sababu mbalimbali za kiuchumi na kijamii.

“ Kiwango cha maambukizi kwa Mkoa wa Mara ni kikubwa kuliko kiwango cha kitaifa cha asilimia 4.5” amesema Bwana Mtaki na kuzitaja sababu ya ongezeko hilo kuwa ni pamoja na uwepo wa shughuli za uchimbaji wa madini, uvuvi na mila na tamaduni za wananchi wa Mkoa wa Mara.

Bwana Mtaki ameeleza kuwa baadhi ya makabila hayafanyi tohara kwa wanaume wakati kiutaalamu tohara inasaidia kuepuka maambukizi ya UKIMWI kwa asilimia 60 na hivyo jamii hizi zipo kwenye hatari ya maambukizi zaidi ya UKIMWI.

Aidha, ameitaja sababu nyingine ni kuwepo kwa mtandao wa ngono ambapo watu wengi wanakuwa na wapenzi zaidi ya mmoja na hivyo kueneza maambukizi ya virusi kwa haraka zaidi.

Wakati huo huo, Mratibu wa Kudhibiti  UKIMWI, Magonjwa ya Ngono na Homa ya Ini Mkoa wa Mara  Dkt. Omari Gamuya ameeleza kuwa Mkoa wa Mara unatekeleza mikakati mbalimbali ili kuhakikisha maambukizi mapya yanapungua katika jamii ikiwemo na kampeni za kutoa elimu katika ngazi ya jamii.

Aidha, Mkoa kwa kushirikiana na wadau umeanza kutoa huduma za dawa tiba kwa kutumia alama za vidole ambayo imesaidia kutoa dawa sahihi

Mafunzo ya Waandishi wa Habari ya siku tatu kuanzia tarehe 11 Desemba, 2023 yamehudhuriwa na Wataalamu kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Shirika la AMREF Afrika na Waandishi wa Habari kutoka baadhi ya vyombo vya Habari vya Mkoa wa Mara.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.