• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Mara yajiandaa kujenga nyumba ya kupumzikia viongozi

Posted on: February 19th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Gerald Musabila Kusaya leo ameiongoza Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara kukagua eneo lilalotarajiwa kujengwa nyumba ya kupumzikia viongozi (rest house) katika eneo la Bweri, Manispaa ya Musoma.

Akizungumza baada ya kupokea maelezo ya wataalamu na kukagua eneo hilo, Bwana Kusaya amewataka wataalamu wanaohusika na ujenzi wa mradi huo kuyachukua maoni yaliyotolewa na Kamati ya Usalama wa Mkoa na kuyafayia kazi kwa haraka.

“Maoni yaliyotolewa na viongozi hapa na yatakayotolewa baadaye yazingatiwe katika mchoro wakati  maeneo halisi majengo yatakayojegwa yanaangaliwa ili kuboresha mchoro uliopo sasa” amesema Bwana Kusaya.

Aidha, Bwana Kusaya amewataka wajumbe wa Kamati ya Usalama ya Mkoa kuendelea kuifikiria michoro ya nyumba hiyo na kama watapata maoni zaidi ya kuboresha wayawasilishe kabla ya ujenzi wa kituo hicho haujaanza ili kuboresha mradi huo.

Kwa upande wake, Katibu Tawala Msaidizi Sehemu ya Miundombinu Mhandishi Richard Moshi amesema michoro ya majengo hayo imeandaliwa na wataalamu kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) na itakuwa na miundombinu yote muhimu kwa ajili ya mahitaji ya sehemu za kupumzikia viongozi.

Mhandisi Moshi amesema ujenzi wa mradi huo unatarajiwa kuanza kutekelezwa katika mwaka wa fedha 2025/2026 na tayari maandalizi muhimu ya mradi huo yamefanyika ikiwa ni pamoja na kutenga bajeti na  kuandaa michoro na kufanya ukadiriaji majenzi ya mradi huo.  

Kwa upande wake, Msanifu Majengo kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mkoa wa Mara Arch. Celestine Kaitaba amesema majengo matano yanatarajiwa kujengwa katika nyumba hiyo ya kupumzikia viongozi.

Arch. Kaitaba amesema michoro ya majengo hayo imezingatia ramani za majengo ya kupumzikia viongozi pamoja na uhalisia wa eneo lenyewe la mradi.

Wakiwa katika eneo hilo pia Kamati ya Usalama imekagua Kituo cha Kulelea watoto cha Musoma na kujionea hali halisi ya kituo hicho kwa sasa.

Katika ziara hiyo Katibu Tawala Mkoa wa Mara ameambatana na Wajumbe wa Kamati ya Usalama Mkoa, Menejimenti ya Sekretarieti ya Mkoa wa Mara na baadhi ya watumishi kutoka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) Mkoa wa Mara.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.