• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

MARA KUTOA ELIMU YA CHAKULA KILICHORUTUBISHWA MASHULENI

Posted on: June 1st, 2021

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bi. karolina Mthapula amewataka wajumbe wa kamati ya lishe pamoja na Elimu Mkoa wa Mara kuhakikisha kuwa elimu kuhusu urutubishaji  wa chakula inasambazwa kwa watoto mashuleni, waalimu, wazazi na wananchi wote kuanzia ngazi ya chini ili kuwepo na uelewa wa umuhimu wa kutumia chakula kilichorutubishwa kwani ni muhimu kwa afya ya watoto.

Bi. Mthapula ametoa kauli hiyo wakati akifungua kikao cha Kamati ya Lishe ya Mkoa pamoja kilichowashirikisha Maafisa Elimu kuhusu urutubishaji wa unga wa mahindi unaozalishwa na viwanda vidogovidogo na kati vilivyopo Mkoani Mara, kikao kilichofanyika leo tarehe 31 Mei2021 katika ukumbi wa Uwekezaji uliopo katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

“Ninaomba wajumbe na wataalamu mliopo hapa tuhakikishe kuwa elimu tunayoipata hapa tunaipeleka kwa  wananchi wote wa Mkoa wa Mara kwani suala la lishe ni suala muhimu kwa afya ya watoto wetu na linapelekea afya ya watoto kuimarika pamoja na kuongezeka kwa  kiwango cha ufaulu mashuleni”.

Aidha amewataka maafisa elimu kuongeza ufanisi katika kutoa elimu ya lishe mashuleni ili watoto wawe na uelewa stahiki ili nao waweze kwenda kupandikiza elimu hiyo majumbani na kwa jamii inayowazunguka.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Mara Dkt. Frolian Tinuga amesema kuwa Mkoa unaendelea kuweka mikakati madhubuti ikiwemo kukutana na wadau pamoja na wazalishaji kujadili namna bora ya utekelezaji wa mwongozo wa kitaifa wa utoaji wa chakula lishe kwa wanafunzi elimu msingi unatumika katika shule zote nchini.

“Kama Mkoa tumedhamiria kusimamia na kuhakikisha Muongozo wa lishe mashuleni unatekelezeka kwa kuhakikisha tunaendelea kuhamasisha, kutoa elimu na kuwajengea uwezo wazalishaji waweze kurutubisha vyakula wanavyozalisha sambamba na kuhakikisha wanafunzi wote mashuleni wanakula chakula kilichorutubishwa” alisema Dkt. Tinuga.

Kwa upande wake, mwakilishi wa ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Bwana Steven Mtambi amesisitiza ulimaji na ulaji wa mahindi ya njano, maharage, viazi, mbogamboga na matunda kwa  shule zenye mazingira yanayowezekana kwani vyakula hivi vina virutubisho ya kutosha na vinasaidia kwa kiwango kikubwa kujenga afya ya watoto.

Bwana Mtambi ameeleza kuwa upungufu wa virutubisho unaweza kusababisha udumavu katika ukuaji wa watoto pamoja na matatizo ya watoto kuzaliwa na mgongo wazi na kichwa kikubwa.

“Asilimia 49% ya watu wa Mkoa wa Mara wana upungufu wa wekundu wa damu unaosababishwa na kukosa lishe bora hivyo nguvu ikiwekezwa katika kuwepo na huduma ya chakula na lishe kwa wanafunzi kutasaidia kuwajengea afya nzuri, kuongeza mahudhuri,kupunguza utoro,kuongeza kiwango cha ufaulu” alisema Bwana Mtambi.

Aidha akimkaribisha Katibu Tawala, Afisa Lishe Mkoa wa Mara Bwana Paul Makali amesema kuwa Mkoa umejipanga kuwajengea uwezo kamati za lishe za Halmashauri ili kuona namna bora ya kuondoa changamoto za lishe katika Mkoa wa Mara.

Bwana Makali amevitaja vyakula vinavyotakiwa kurutubishwa kuwa ni chumvi, mafuta ya kula, unga wa mahindi pamoja na unga wa ngano.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.