• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Magari haya yatumike kuwahudumia wananchi: Mtambi

Posted on: July 12th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 11 Julai, 2024 amekabidhi magari yaliyotolewa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwa Wakuu wa Wilaya na kuwataka kutumia magari hayo katika kuwahudumia wananchi.

Akizungumza katika hafla fupi ya makabidhiano ya magari hayo Mhe. Mtambi amemshukuru Mhe. Rais kwa kuwapatia Wakuu wa Wilaya Magari hayo ambayo yatawasaidia kuwafikia wananchi na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yao.

“Magari haya yatumike kwa mujibu wa maelekezo ya Serikali ya kusikiliza na kutatua kero za wananchi  na kukagua miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika maeneo yenu” amesema Mhe. Mtambi.

Aidha, amewataka Wakuu wa Wilaya kuhakikisha magari hayo yanatunzwa na kuwekwa katika hali nzuri ili yadumu na kutoa huduma kwa wananchi kwa muda mrefu.

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Gerald Musabila Kusaya ameeleza kuwa katika awamu hii, Wakuu wa Wilaya za Bunda, Serengeti na Rorya ndio wamepewa magariyaliyopangwa katika bajeti ya mwaka 2023/2024.

Bwana Kusaya amesema Wakuu wa Wilaya za Musoma, Tarime na Butiama wanatarajiwa kupatiwa magari katika bajeti ya mwaka wa fedha 2024/2025.

Bwana Kusaya amemuomba Mkuu wa Mkoa kuyazindua na kuyakabidhi magari hayo ili yaanze kutumika katika kuwahudumia wananchi wa wilaya hizo.  

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Serengeti Mhe. Dkt. Vincent Mashinji amemshukuru Mhe. Rais kwa kutoa magari hayo na kuondoa changamoto ya magari waliyokuwa nayo katika utekelezaji wa majukumu yao.

Dkt. Mashinji amesema magari hayo yatawasaidia kuwatembelea na kusikiliza kero za wananchi na kukagua miradi ya maendeleo iliyopo katika Wilaya zetu na kuwataka madereva kuyatunza magari hayo ili yaweze kudumu muda mrefu.  

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.