• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

LAAC yapongeza ujenzi Sekondari ya Nyasaricho

Posted on: March 21st, 2024

Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC) leo imefanya ziara katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na kuelezea kuridhishwa kwake na mradi wa ujenzi wa Shule ya Sekondari ya Nyasaricho.

Akizungumza katika kikao cha majumuisho, Makamu Mwenyekiti wa LAAC Mhe. Stanslaus Mabula ambaye ameongoza msafara huo ameeleza kuwa ujenzi wa mradi huo umesimamiwa vizuri na shule hiyo imewekwa katika mazingira mazuri na ya usafi.

“Ninampongeza Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Nyasaricho kwa kuweka mazingira vizuri na katika hali ya usafi na ninamuombea aendelee kuwepo katika shule hii kwa maana anastahili” amesema Mhe. Mabula.

Aidha, ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Tarime kwa usimamizi mzuri wa mradi huo na kuwataka mameneja wa Wilaya wa TANESCO na RUWASA kuhakikisha kuwa huduma za maji na umeme zinafika katika Shule ya Sekondari ya Nyasaricho.   

Akizungumzia kuhusu jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, Mhe. Mabula ametoa miezi mitatu kwa mkandarasi wa jengo hilo SUMA JKT kurudia rangi baadhi ya sehemu na kufanya usafi wa rangi zilizomwagika maeneo mbalimbali wakati wa umaliziaji wa jengo hilo.

Mhe. Mabula ameiagiza Halmashauri hiyo kununua samani za ofisi zinazendana na jengo hilo haraka iwezekanavyo ili watumishi waweze kufanya kazi katika mazingira mazuri.

Akizungumzia kuhusu samani za jengo la ofisi, Mkurugenzi wa Halmashauri hiyo Bwana Solomon Shati ameeleza kuwa tayari Halmashauri imetenga fedha shilingi milioni 300 kwa ajili ya ununuzi wa samani katika mwaka wa fedha 2023/2024.

“Tayari matangazo ya kutafuta wazabuni wa kutengeneza samani hizo yapo kwenye mfumo wa ununuzi wa NEST, na taratibu za manunuzi zikikamilika, kutakuwa na samani mpya katika ofisi zote za jengo hilo” amesema Bwana Shati.

Bwana Shati ameahidi kumsimamia mkandarasi kukamilisha shughuli zilizobakia pamoja na kufanya usafi wa jengo hilo ndani ya muda mfupi kabla ya malipo yao ya mwisho kwa ajili ya kazi hayajafanyika.    

Aidha, wabunge mbalimbali wamechangia kuhusu ziara hiyo wamepongeza ujenzi na usimamizi wa shule hiyo huku Mbunge wa Jimbo Serengeti Mhe. Amsabi Mrimi akiishauri Halmashauri kuongeza eneo la shule hiyo na kupanda miti ya kivuli kuzunguka shule hiyo ili wanafunzi wapate eneo zuri kwa ajili ya kujisomea.

Baadhi ya wabunge pia wameiomba Halmashauri kuhakikisha inaweka umeme katika shule hiyo ili watumishi na wanafunzi waweze kukaa maeneo mazuri na kuweza kujisomea kiurahisi.

Kamati hiyo leo imetembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la utawala la Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na Shule ya Sekondari ya Nyasarisho katika Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na kesho  Kamati ya LAAC itatembelea na kukagua mradi wa ujenzi wa jengo la utawala na soko la kimkakati katika Halmashauri ya Mji wa Tarime.

Shule ya Sekondari ya Nyasaricho imejengwa baada ya Halmashauri kupokea shilingi bilioni 1 wa kujenga shule ya bweni kwa ajili ya wanafunzi wa kutwa kidato cha kwanza hadi cha nne na wanafunzi wa bweni kidato cha tano na sita ambapo Halmashauri pia imeongezea shilingi milioni 600,000 kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa shule hiyo.

Ziara hiyo imehudhuriwa pia na Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Bwana Wilson Charles Mahera,  Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Gerald Musabila Kusaya, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Tarime, maafisa kutoka TAMISEMI, Ofisi ya Bunge, Wizara ya Fedha, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na kadhalika.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.