• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Kusaya awataka wahanga kutumia misaada kuboresha maisha

Posted on: May 19th, 2025

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Gerald Musabila Kusaya amewataka wananchi waliopata madhara yaliyosababishwa na mvua iliyoambatana na upepo katika Manispaa ya Musoma tarehe 23 Machi, 2025 kutumia misaada wanayopewa kuboresha maisha yao.

Akizungumza katika hafla ya kukabidhi misaada kwa wahanga amewataka kutumia misaada hiyo kwa malengo yaliyokusudiwa ili kuboresha maisha yao baada ya tatizo hilo lililowapata.

“Msaada mtakaopokea leo msiende kutumia ovyo, mtumie kulingana na malengo ya misaada hiyo katika kuboresha maisha yenu baada ya masaibu yaliyowakuta” amesema Bwana Kusaya.

Bwana Kusaya amemshukuru Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan na Ofisi ya Waziri Mkuu kwa kutoa fedha na vifaa kama vile mabati, magodogo, mablanketi, ndoo kwa ajili ya waathirika hao.

Aidha, amewashukuru Mbunge wa Viti Maalum Ghati Chomete, Mbunge wa Jimbo la Musoma Mjini Mhe. Vedastus Mathayo, Nyansaho Foundation, mgodi wa Barrick North Mara na wadau wengine waliotoa msaada kwa waathirika hao kwa nyakati tofauti.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mkuu wa Wilaya ya Mara Mhe. Juma Chikoka amesema anaishukuru Serikali na wadau wote waliochangia katika maafa hayo na kuwashukuru wananchi kwa ustahimilivu wao wakati Serikali ilipokuwa inatoa msaada kwa makundi mbalimbali kulingana na uathirika wao.

Mhe. Chikoka amewahakikishia wananchi hao kila mmoja aliyeathirika atafikiwa na Serikali na kupewa msaada kulingana na kiasi cha fedha na mali zilizopo.

Mhe. Chikoka amewataka wananchi kuendelea na shughuli zao za maendeleo kwa amani na utulivu wakati huu nchi inapoelekea katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na kuwahakikishia kuwa usalama wakati wote wa uchaguzi.

Kwa upande wake, Mratibu wa Maafa Manispaa ya Musoma Bibi Aines Anderson amesema katika maafa hayo nyumba 196 ziliathirika na kusababisha kaya 139 kukosa makazi na kaya 16 zenye watu 40 zilihifadhiwa katika majengo ya NFRA na kuhudumiwa kwa chakula na malazi kwa siku tatu kabla ya kupewa pesa za pango la miezi sita kwa kila kaya.

Bibi Aines Anderson amesema tangu kutokea kwa maafa hayo, jumla ya nyumba sita za wazee na watu wasiojiweza zimejengwa katika kata za Nyakato, Kitaji, Kwangwa na Rwamlimi na kukarabati nyumba 33 katika kata za Kitaji na Nyakato.  

Amesema msaada unaogawiwa leo ni mabati 568 kwa ajili ya kaya 29, magodoro 91 na mablanketi 100 yaliyotolewa kwa ajili ya kaya 91 na saruji mifuko 70 iliyotolewa kwa ajili ya jengo la kilimo na Shule ya Msingi Mwembeni B zilizoathirika katika tukio hilo.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • RC atoa siku 14 wanafunzi wote Sekondari ya J. K. Nyerere wapate chakula shuleni

    July 28, 2025
  • Kusaya apokea ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama

    July 25, 2025
  • Mtambi ataka matumizi ya GOTHOMIS kwa asilimia 100 Mara

    July 25, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.