• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Kusaya awaalika wananchi kushiriki Maadhimisho ya Wazee

Posted on: June 6th, 2024

Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Gerald Kusaya amezungumza na waandishi wa habari kuhusu Maadhimisho ya Siku ya Kupinga Ukatili dhidi ya Wazee ambayo kitaifa yanatarajiwa kufanyika katika Wilaya ya Bunda, Mkoa wa Mara tarehe 13-15 Juni, 2024.

Bwana Kusaya amesema maadhimisho hayo yanatarajiwa kuanza kufanyika tarehe 13 Juni, 2024 kwa wazee kushiriki michezo mbalimbali itakayofanyika katika Shule ya Sekondari ya Bunda na zoezi la kupima afya litakalofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Miembeni.

“Zoezi la kupima afya kwa wazee wote litakuwa bure na litafanywa na wataalamu wetu wa afya waliopo katika Mkoa wa Mara na wazee watapatiwa matibabu katika viwanja hivyo” amesema Bwana Kusaya.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, tarehe 14 Juni, 2024 kutakuwa na kongamano litakalojadili masuala mbalimbali ya Wazee ambalo litafanyika Chuo cha Ualimu Bunda na kufuatiwa na ziara ya Wazee nyumbani kwa Baba wa Taifa  Mwalimu Julius Kambarage Nyerere.

Bwana Kusaya amesema kilele cha maadhimisho hayo itakuwa ni tarehe 15 Juni, 2024 na mgeni rasmi anatarajiwa kuwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wananwake na Makundi Maalum Mhe. Dkt. Dorothy Gwajima (Mb.).

Bwana Kusaya amesema kauli mbiu ya maadhimisho hayo mwaka huu ni: Utu, Usalama na Ustawi ni nyenzo ya Kutokomeza vitendo vya Ukatili dhidi ya Wazee na kuwaomba wananchi wote kujitokeza kushiriki katika matukio mbalimbali ya maadhimisho haya.

Bwana Kusaya amezungumza na Waandishi wa Habari baada ya kuhitimisha kikao cha tatu cha maandalizi kilichowahusisha viongozi, watumishi wa umma na wadau mbalimbali kilichofanyika katika ukumbi wa Herieth uliopo katika Mji wa Bunda.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.