• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Kikwete achangisha milioni 200 za ujenzi wa kanisa Mara

Posted on: May 26th, 2025

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mstaafu, Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Mei 25, 2025 ameongoza harambee katika Kanisa la Mtakatifu Petro, Parishi ya Bunda, Dayosisi ya Mara ya Kanisa la Angikana la Tanzania na kufanikisha kukusanya shilingi milioni 205.

Akizungumza katika harambee hii iliyofanyika katika Ukumbi wa Chuo cha Ualimu Bunda, Mhe. Dkt. Kikwete amewaomba Watanzania kuendelea kuwa na mshikamano wa Kitaifa kama ilivyo desturi ya kutobaguana, ndiyo maana na yeye japokuwa ni Muisilamu lakini amekuja kuongoza Harambee ya ujenzi wa Kanisa la Mtakatifu Petro ili kanisa hilo linafanane na heshima ya Mtakatifu Petro ilivyo.

“Kweli Kanisa lenu lile ni dogo hata Mtakatifu Petro huko alipo atakuwa anasikitika, lazima lijengwe kanisa la kubwa lenye hadhi yake na ndiyo maana na mimi nipo hapa” amesema Mhe. Kikwete.

Mhe. Dkt. Kikwete amesema watu wa Mkoa wa Mara ni wakalimu na wanapenda watu hata mdogo wake aliwahi kuoa Mkoani Mara, huku akisimulia kuwa yeye binafsi anaujamaa wa karibu na watu wa Mkoa huu.

Akizungumza wakati wa kumkaribisha Dkt. Kikwete, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi amesema hali ya Mkoa wa Mara ni salama na tulivu, huku wakiendelea kusimamia miradi kadhaa ya maendeleo kutoka Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan.

Mhe. Mtambi amemkaribisha na kumshukuru Mhe. Kikwete kwa kutembelea na kuongoza harambee hiyo katika Mkoa wa Mara.

Mhe. Mtambi ametumia pia fursa hiyo kuwakumbusha waumuni wa Kanisa la Anglikana kuwahamasisha wananchi kuhusu kushiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 kwa amani na utulivu.

Kwa upande wao viongozi wa Kanisa la Anglikana Dayosisi ya Mara na Dayosisi kando kando walioshiriki Harambee hii wamemshukuru Dkt. Kikwete kwa kuongoza na kufanikisha kupatikana pesa hizo.

Katika harambee hiyo, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan amechangia shilingi milioni 50 wakati Mkuu wa Mkoa wa Mara akichangia shilingi milioni 15 katika harambee hiyo.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • RC atoa siku 14 wanafunzi wote Sekondari ya J. K. Nyerere wapate chakula shuleni

    July 28, 2025
  • Kusaya apokea ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama

    July 25, 2025
  • Mtambi ataka matumizi ya GOTHOMIS kwa asilimia 100 Mara

    July 25, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.