• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Kamati ya Usalama ya Mkoa yakagua miradi ya Mwenge

Posted on: July 9th, 2024

Kamati ya Usalama wa Mkoa wa Mara inayoongozwa na Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo imeanza ziara ya kutembelea na kukagua miradi itakayofikiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024 kwa kufanya ziara Halmashauri ya Manispaa ya Musoma na Halmashauri ya Wilaya ya Musoma.

Kamati hiyo ikiwa katika Manispaa ya Musoma, imetembelea na kukagua  jengo la kupumzika abiria katika eneo la Mwigobero lililojengwa na Wakala wa Umeme na Ufundi (TEMESA) na baadaye kuwasalimia na wananchi waliokuwa wamepanda kivuko tayari kuelekea eneo la Kinesi, Wilaya ya Rorya.

Kamati hiyo pia ametembelea na kukagua Zahanati ya Mshikamano ambayo ujenzi wake ulianzishwa kwa nguvu za wananchi na baadaye Serikali kuu na Halmashauri kukamilisha ujenzi huo na kutembelea daraja la Ngaranjabo linalounganisha Kata ya Buhare na Kata ya Makoko linalojengwa na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA).

Baada ya hapo, Kamati imeelekea  Halmashauri ya Wilaya ya Musoma ambapo ametembelea na kukagua ujenzi wa Zahanati ya Mmahare, ujenzi wa mradi wa maji wa Chumwi Mabuyi unaotekelezwa na Wakala wa Maji Vijijini (RUWASA).

Katika ziara hiyo, Mhe. Mtambi amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kuyafanyia kazi maekelezo ya Kamati ya Wataalamu na Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara kuhusu marekebosho yanayohitaji kufanyika katika miradi yote itakayotembelewa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2024.

Wakati huo huo, akiwa katika tenki la mradi wa maji wa Chumwi Mabuyi, Mkuu wa Mkoa wa Mara ameagiza kukarabatiwa kwa Shule ya Msingi Mabume Rafuru ambayo ipo jirani na tenki la mradi wa maji wa Chumwi- Mabuyi  ambayo ina majengo mengi yaliyochakaa sana na mazingira yasiyoridhisha.

Mhe. Mtambi ameelekeza sehemu ya mchango wa mwenge wa Wilaya ya Musoma kukarabati shule hiyo ikiwa ni pamoja na kuboresha ofisi ya walimu na kuweka samani katika ofisi ya Mwalimu Mkuu wa shule hiyo na kubomoa vyoo vya zamani ambavyo havitumiki vilivyopo katika eneo hilo kwa kuwa ni hatarishi kwa watoto na vinachafua mazingira.  

Mhe. Mtambi amemuagiza Katibu Tawala wa Mkoa kuongeza nguvu katika ukarabati wa shule hiyo na kuhakikisha ukarabati huo unakamilika ili wanafunzi wajivunie kufikiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru katika shule yao.

Kanali Mtambi ameitaka Kamati ya Wataalamu ya Ukaguzi wa Miradi ya Mwenge Mkoa wa Mara kukagua maendeleo ya ukarabati wa shule hiyo tarehe 21 Julai, 2024 na kutoa taarifa kuhusu utekelezaji wa maagizo hayo.

Katika ziara hiyo, Kamati ya Usalama ya Mkoa iliambatana na Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Musoma, baadhi ya maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Wakuu wa Taasisi na baadhi ya maafisa wa Halmashauri za Manispaa ya Musoma na Halmashauri  ya Wilaya ya Musoma.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.