• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Hapi: Mkawatumikie Wananchi

Posted on: June 22nd, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Ally Salum Hapi leo tarehe 21 Juni 2021 amewaapisha Wakuu wa Wilaya wanne wapya walioteuliwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan tarehe 19 Juni 2021.

Akizungumza wakati wa kuawaapisha wakuu wa wilaya hao, Mheshimiwa Hapi amewataka kwenda kusimamia miradi ya serikali inayotekelezwa katika wilaya zao ili wananchi waweze kupata manufaa ya miradi hiyo kama ilivyokusudiwa.

“Wananchi  wamekipa dhamana Chama cha Mapinduzi (CCM) wakiamini kitawaletea maendeleo na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili na CCM ikaunda serikali ya Rais aliyewatuma kumwakilisha huku kutatua kero za wananchi wa Mkoa wa Mara, sasa tukachape kazi” alisema Mheshimiwa Hapi.

Amewataka Wakuu wa Wilaya kutumia asimilia 70 ya muda wao wakiwa kwenye kukagua miradi na kusikiliza kero za wananchi na kutumia asilimia 30 tu ya muda wao kukaa ofisini.

“Ninataka mtenge muda na siku maalum mkiwa na wataalamu wenu ili kusikiliza kero za wananchi wa wilaya zenu na kutatua baadhi ya kero za wananchi mtakazoweza na ambazo mtaona mnahitaji msaada kuzitatua tupo tayari kusaidiana kuweza kuzitatua ” alisema Mheshimiwa Hapi.   

Aidha Mheshimiwa Hapi amewataka viongozi hao kusimamia haki za wananchi wanyonge pamoja na watumishi waliopo katika maeneo yao hususan wanaoishi maeneo ya vijijini .

“Mhakikishe kuwa Maafisa Utumishi wanaenda kuwasikiliza watumishi mbalimbali waliopo katika maeneo yenu,  ili watumishi wawatumikie wananchi wakiwa na furaha na wananchi nao wahudumiwe wakiwa na furaha” alisema Mheshimiwa Hapi.

Amewataka kutilia mkazo zaidi katika sekta za huduma za jamii hususan elimu, afya, maji na umeme ambazo zinawaathiri wananchi wangi katika maeneo yao. 

Kwa upande wake Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Albert Gabriel Msovela amewapongeza Wakuu wa Wilaya hao kwa kuaminiwa na Mheshimiwa Rais ili waweze kusimamia wilaya hizo.

Aidha amewataka Wakuu wa Wilaya hao kufuata sheria, kanuni na taratibu zilizopo katika utendaji kazi wao ikiwemo ya utoaji wa taarifa nje ya Mkoa.

“Ninawaomba mkawatumie vizuri wataalamu na vyombo vya ulinzi na usalama vilivyopo chini yetu kwa ajili ya kuwashauri na kuwapa utaalamu unaohitajika katika utekelezaji wa majukumu yenu” alisema Bwana Msovela.

Wakuu wa Wilaya walioapishwa leo ni Mheshimiwa Dkt. Vincent Mashinji  kuwa Mkuu wa Wilaya ya Serengeti;  Mheshimiwa Juma Issa Chokoka kuwa Mkuu wa Wilaya ya Rorya; Mheshimiwa Joshua Samweli Nassari Mkuu wa Wilaya ya Bunda na Mwalimu Moses Rudovick Kaengele Mkuu wa Wilaya ya Buatiama.

Wengine ambao Mheshimiwa Rais amewahamishia katika Mkoa wa Mara ni Mhe. Dkt. Halfan Haule Mkuu wa Wilaya ya Musoma na Lt. Col. Michael Mangwela Mtenjele Mkuu wa Wilaya ya Tarime. 

Shughuli ya uapisho huo umehudhuriwa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara Mheshimiwa Samweli Kiboye, Viongozi wa Dini, Makatibu Tawala wa Wilaya, Meya wa Mji wa Musoma, Wenyeviti wa Halmashauri, Wakurugenzi wa Halmashauri pamoja na watumishi , viongozi wa taasisi mbalimbali za serikali na za binafsi pamoja na wananchi wa Mkoa wa Mara.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.