• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Hapi azindua Kampeni ya Usafi Mara

Posted on: September 4th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Ally Salum Hapi le tarehe 4 Septemba 2021 amezindua Kampeni ya Usafi wa Mazingira kwa Mkoa wa Mara kwa kufanya usafi katika Soko Kuu la Musoma na baadaye kushiriki kufanya usafi katika Soko la Saanane.

Akizungumza na wananchi na wafanyabiashara wa Soko la Saanane Mheshimiwa Hapi amewashukuru wananchi waliojitokeza kufanya usafi katika eneo hilo.

“Ninawashukuru sana kwa kuja na kushiriki katika kufanyausafi kwa wingi namna hii, zoezi hili litakuwa ni zoezi endelevu hivyo tuendelee kuyasafisha mazingira tunayoyatumia” alisema Mheshimiwa Hapi.

Aidha amewataka viongozi wa mitaa, kata na vijiji kuendelea kuwasimamia wananchi katika kufanya usafi wakati wote katika maeneo yao ili kuweza kupunguza magonjwa yanayotokana na usafi.

Mkuu wa Mkoa amewaagiza wafanyabiashara kuendelea kufanya usafi katika maeneo yanayozunguka biashara zao ili kufanyabiashara katika maeneo masafi kwa aili ya kulinda afya zao na afya za wateja wao.

Mheshimiwa Hapi ameahidi kuwaletea seti moja ya televisheni ili wafanyabiashara hao waweze kuangalia taarifa za habari wakati wanaendelea na biashara zao.

Amewahimiza wazazi kuwafundisha watoto usafi ili wajifunze wakiwa bado wadogo thamani ya usafi katika maisha yao na jamii nzima.

Mheshimiwa Hapi amesema hivi karibuni Mkoa utazindua kampeni ya kupanda miti katika maeneo mbalimbali na wananchi watagawiwa miche ya kupanda katika maeneo ya nyumba zao.     

Akizungumza wakati wa kumkaribisha Mkuu wa Mkoa, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Dkt. Alfany Haule ameeleza kuwa katika Wilaya ya Musoma usafi umefanyika katika kata zote za Wilaya ya Musoma na mwitikio wa wananchi umekuwa mkubwa sehemu zote.

“Tumejipanga kuhakikisha wilaya yetu inaondokana na magonjwa yanayotokana na uchafu ambayo yanawaathiri wananchi wetu kwa kusimamia usafi wa mazingira yanayotuzunguka” alisema Mheshimiwa Haule.

Ameeleza kuwa japokuwa kampeni ya usafi imezinduliwa katika Wilaya ya Musoma, zoezi la usafi limefanyika leo katika wilaya zote za Mkoa wa Mara.

Amewashukuru sana wananchi kwa kujitokeza kwa wingi ili kufanikisha uzinduzi wa kampeni ya usafi.  

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.