• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Hapi atoa wiki mbili kukamilisha miradi

Posted on: July 15th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Ally Salum Hapi ameiagiza Sekretariati ya Mkoa wa Mara kukamilisha miradi mine ya ujenzi na ukarabati wa nyumba za viongozi wa huu inayotekelezwa katika Manispaa ya Musoma.

Mheshimiwa Hapi ametoa maagizo hayo leo tarehe 14 Julai 2021 katika ziara yake aliyoifanya kukagua miradi mine inayotelekelezwa kwa mfumo wa force account na kusimamiwa na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara katika Manispaa ya Musoma.

“Ninatoa wiki mbili miradi hii minne yote iwe imekamilika…..ninataka ofisi yangu iwe ni ofisi ya mfano katika utekelezaji wa miradi ya serikali katika Mkoa wa Mara” alisema Mheshimiwa Hapi.

Akizungumza baada ya kukagua miradi hiyo, Mheshimiwa Hapi ameeleza kuwa hajaridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi, usimamizi na ugawaji wa kazi kwa mafundi wa miradi hiyo ambao wanaajiri mafundi wengine katika utekelezaji na hivyo kuchelewesha utekelezaji wa miradi hiyo.

Aidha Mkuu wa Mkoa ameagiza kupatiwa taarifa ya kina kuhusu matumizi ya fedha na hususan fedha zilizotumika katika manunuzi ya vifaa na kulipa mafundi katika miradi hiyo.  

Awali akitoa taarifa ya miradi hiyo Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Miundombinu Mhandisi Faustin Tarai ameeleza kuwa miradi hiyo ilianza kutekelezwa kuanzia tarehe 15 Machi 2021 na inatarajiwa kukamilika tarehe 19 Julai 2021.

Aidha Bwana Tarai ameeleza kuwa kuwa vifaa vyote kwa ajili ya miradi hiyo vilishanunuliwa na malipo ya mafundi yanaendelea kutolewa kulingana na madai wanayoyatoa baada ya kukamilisha sehemu ya kazi.

Katika kukagua miradi hiyo Mkuu wa Mkoa aliambatana na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Albert Gabriel Msovela; Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mheshimiwa Alfany Haule, Wakuu wa Idara na Vitengo kutoka Sekretariati ya Mkoa, wataalamu wa ofisi ya Katibu Tawala Wilaya ya Musoma pamoja na waandishi wa habari.

Miradi inayotekelezwa na Sekretariati ya Mkoa wa Mara katika Manispaa ya Musoma ni pamoja na  ujenzi wa nyumba ya Katibu Tawala Msaidizi sehemu ya Afya; ujenzi wa nyumba ya Katibu Tawala wa Wilaya ya Musoma; ukarabati wa nyumba ya Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara;  na ukarabati wa nyumba ya Mkuu wa Wilaya ya Musoma ambayo imefikia katika hatua tofauti za ukamilishaji wake.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • RC atoa siku 14 wanafunzi wote Sekondari ya J. K. Nyerere wapate chakula shuleni

    July 28, 2025
  • Kusaya apokea ofisi ya Mkuu wa Wilaya ya Butiama

    July 25, 2025
  • Mtambi ataka matumizi ya GOTHOMIS kwa asilimia 100 Mara

    July 25, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.