• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Acheni Tegesha -Mtambi

Posted on: May 25th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo ameendelea na ziara yake katika Wilaya ya Serengeti ambapo ametembelea Chuo cha Mamlaka ya Ufundi Stadi (VETA) kinachooendelea kujengwa katika Kata ya Uwanja wa Ndege na kuwataka wananchi wa Mkoa wa Mara kuacha kufanya tegesha inakwamisha maendeleo na kupandisha gharama za mradi wa maendeleo.  

Mhe. Mtambi ametoa kauli hiyo baada ya baadhi ya wakazi wa eneo la Burunga kudai kuwa  maeneo yao yamechukuliwa bila kufuata utaratibu na kujenga Chuo cha VETA na mpango wa Serikali kuhamisha barabara inayopita eneo hilo kupisha ujenzi wa Uwanja wa Ndege wa Mugumu mambo ambayo yamethibitishwa katika kikao hicho kuwa sio kweli.

 “Serikali haitamvumilia mtu yoyote anayekwamisha mradi wa maendeleo kwa ajili ya manufaa yake  binafsi na tutamchukulia hatua mtu yoyote atakayefanya hivyo” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Serengeti kufuatilia taarifa kuwa  Wakala wa Barabaraa (TANROADS) Mkoa wa Mara iliwazuia wananchi hao kuendeleza maeneo yao kuanzia mwaka 2010 hadi sasa na tayari wameshafanyiwa tathmini tangu mwaka 2019.  

Kwa upande wake, aliyekuwa Mwenyekiti wa Kijiji hicho Bwana Mateso Moses Kairo amesema awali, eneo hilo lilikuwa la Kijiji cha Burunga ekari 72 na Kijiji kiliamua kulitoa kwa Serikali kwa ajili ya ujenzi wa Chuo cha VETA.

Bwana Kairo amesema kuwa baadaye baada ya mawasiliano na Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti, VETA ilipewa eneo la ekari 42 na ekari 10 walipewa Shirika la Kuhudumia Viwanda Vidogo vidogo (SIDO) na eneo lililobakia limekuwa ni mali ya kijij hicho.

Bwana Kairo amesema baada ya Serikali ya Kijiji kuvunjwa na eneo hilo kuingizwa kwenye Mamlaka ya Mji, baadhi ya wananchi wasiokuwa waaminifu walilivamia eneo hilo na kudai ni mali yao na wengine kuwauzia wageni waliokuwa wanatafuta maeneo.

Amesema kuwa wananchi waliovamia eneo hio walifungua kesi kwenye Baraza la Ardhi la Kata na Baraza la Ardhi la Wilaya ambapo wameshindwa lakini bado wakija viongozi maeneo hayo wanadai eneo hilo ni lao, vielelezo vya uhalali wa eneo hilo vipo na ndio vilipelekwa mahakamani.

Awali, wananchi wawili walijitokeza kudai fidia kutokana na maeneo yao kuchukuliwa kupisha mradi WA Chuo cha VETA na ujenzi wa barabara ya Wakala wa Barabara nchini (TANROADS) jambo ambalo lilikuja kuthibitishwa katika kikao hicho kuwa sio sahihi.

Mkuu wa Mkoa amezungumza na wananchi waliokuwepo eneo la ujenzi wa Chuo cha VETA ambapo alitumia nafasi hiyo kusikiliza kero zao na kuzitolea ufafanuzi.

 Katika ziara hiyo Mkuu wa Mkoa aliambatana na baadhi ya Wajumbe wa Kamatiya Usalama ya Mkoa, Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Serengeti, Viongozi wa Chama cha Mapinduzi, Mwenyekiti na Menejimenti ya Wilaya ya Serengeti na maafisa kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, taasisi na Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti.

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.