Mwenge wa Uhuru umeingia leo Mkoani Mara ukitokea Wilaya ya Ukerewe Mkoani Mwanza. Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru yamefanyika katika kijiji cha Kisorya Wilaya Bunda Mkoa wa Mara. Ukiwa Mkoani Mara Mwenge wa Uhuru utakimbizwa siku tisa katika Halmashauri zote tisa za Mkoa wa Mara. Mwenge wa Uhuru utaweka mawe ya msingi, kukagua, kuzindua na kufungua jumla ya miradi 61 yenye thamani ya shilingi bilioni 10,959,532,585. Mwenge wa Uhuru utakabidhiwa Mkoa wa Arusha tarehe 01/09/2017 katika Kijiji cha Ololosikwani Wilaya ya Ngorongoro.
Kauli Mbiu ya Mwenge wa Uhuru mwaka 2017 ni " SHIRIKI KUKUZA UCHUMI WA VIWANDA KWA MAENDELEO YA NCHI YETU".
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Simu: +255282622305
Simu:
Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz
Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa