• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Mipango na Uratibu
      • Sekta ya Elimu
      • Huduma ya Maji
      • Uchumi na Uzalishaji
      • Utawala na Rasilimali Watu
      • Afya na Ustawi wa Jamii
      • Huduma za Serikali za Mitaa
      • Miundombinu
    • Vitengo
      • Huduma za Kisheria
      • Uhasibu na Fedha
      • Ukaguzi wa Ndani
      • Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Ugavi na Manunuzi
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Zingatieni miongozo ya kilimo cha tumbaku- Dkt. Haule

Posted on: June 18th, 2025

Mkuu wa Wilaya ya Rorya Mhe. Dkt. Khalfan Haule amewataka wadau wa zao la tumbaku kuzingatia miongozo na kanuni za kilimo cha zao la tumbaku ili kuongeza uzalishaji na kuboresha hali ya wakulima wa zao hilo.

Mhe. Haule ametoa kauli hiyo wakati wa mkutano wa kwanza wa wadau wa zao la tumbaku uliowaleta pamoja wakulima, wanunuzi, wawakilishi wa Serikali na taasisi za kifedha katika Mkoa wa Mara uliofanyika tarehe 17 Juni, 2025 katika Hoteli ya Kisare iliyopo katika Mji wa Mugumu, Wilaya ya Serengeti.

“Mafanikio katika kilimo cha tumbaku yanategemea sana kufuatwa kwa taratibu za ulimaji na uvunaji wa zao hilo ili kuleta manufaa makubwa kwa mkulima kama inavyokusudiwa, bila hivyo wakulima watakuwa wanahangaika tu bila mafanikio” amesema Dkt. Haule.

Dkt. Haule amesema kwa kuzingatia kanuni na miongozo itawasaidia wakulima kuepusha hasara, kupunguza magonjwa ya mimea na kuongeza mavuno kwa ekari, jambo ambalo litawawezesha wakulima kunufaika zaidi na jasho lao.

Dkt. Haule amesema Serikali imetenga fedha nyingi kwa ajili ya ruzuku katika zao la tumbaku hivyo amewasisitiza wadau wote kusimamia miongozo ya kitaalamu ya kilimo cha tumbaku kuanzia kupanda, utunzaji, uvunaji, ukusanyaji wa tumbaku ili kupata tumbaku bora inayokidhi viwango vya ndani na nje ya nchi.

Lengo la mkutano huo wa wadau ni kuboresha uzalishaji wa tumbaku, kuboresha upatikanaji wa masoko na ustawi wa wakulima wa zao hilo na kutafuta suluhu ya changamato zinazoikabili kilimo cha tumbaku katika Mkoa wa Mara.

Mhe. Haule ametumia fursa hiyo kukemea tabia ya utoroshaji wa tumbaku kuelekea nchi jirani na kuwatahadhalisha wadau hao kuwa hatua kali za kisheria zitachukuliwa kwa watakaobainika kutorosha tubaku katika Mkoa wa Mara. 

Aidha, Dkt. Haule amewataka wanunuzi wa tumbaku na taasisi zinazotoa pembejeo kutoa elimu sahihi na endelevu kwa wakulima wa zao la tumbaku ili wakulima waweze kufaidika na kilimo cha tumbaku na kuendeleza uchumi wao binafsi na Taifa lao.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Wakulima wa Mara Cooperative Union (WAMACU) LTD Bwana Momanyi Range ameomba ushirikiano baina ya Serikali, wakulima na wataalam ili zao la tumbaku liweze kuwa na tija kwa pande zote.

Bwana Range amesema kwa sasa wakulima wameitikia kulima tumbaku na hususan katika Wilaya ya Serengeti na kuwaomba wadau kuendelea kutoa elimu ili wakulima waweze kuboresha uzalishaji wa tumbaku na wananchi wengi zaidi waweze kulima tumbaku katika Mkoa wa Mara.

Matangazo ya Kawaida

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mara mshindi wa pili UMITASHUMTA 2025

    June 18, 2025
  • Zingatieni miongozo ya kilimo cha tumbaku- Dkt. Haule

    June 18, 2025
  • Mtambi aipongeza Bunda TC kwa hati safi miaka mitano mfululizo

    June 13, 2025
  • Mtambi aitaka Bunda DC kuwasilisha Mkakati wa kukusanya milioni 700

    June 13, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa