• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi ataka maboresho utoaji wa mikopo ya asilimia 10

Posted on: August 6th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo ameongoza kikao cha pili cha maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru, 2025 katika Mkoa wa Mara na kutaka maboresho ya utoaji wa mikopo ya Halmashauri inayotolewa kwa vikundi mbalimbali katika kijamii.

Mhe. Mtambi amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuwa wabunifu katika utoaji wa mikopo hiyo ili kuongeza tija ya mikopo hiyo kwa vikundi ambavyo vinastahili mikopo hiyo na kupiga marufuku mikopo kwa ajili ya biashara za kubeba abiria kwa kutumia pikipiki (bodaboda).

“Kuanzia sasa ninataka kuona mikopo inatolewa kwa vikundi ambavyo vitafanya biashara endelevu ya uzalishaji mali, zenye tija na zinazoonyesha ubunifu na sio kila kikundi biashara ni ya boda boda” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii wa Halmashauri za Mkoa wa Mara kuwahamasisha wananchi kubuni miradi mizuri yenye tija, endelevu na inayoweza kuboresha uchumi wa jamii na Halmashauri husika.

Mhe. Mtambi ametoa mfano wa biashara za ufugaji wa samaki katika vizimba, kilimo cha umwagiliaji kulingana na maeneo mikopo hiyo inapotolewa ili kuwahamasisha kutumia ubunifu kulingana na mazingira waliyonayo katika Halmashauri husika.  

Kanali Mtambi amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara kuanzisha vikao vya kila robo mwaka vya sekta za uzalishaji mali, biashara na Maafisa Maendeleo ya Jamii kwa ajili ya kupata taarifa ya mikopo iliyotolewa na Halmashauri na fursa zilizopo katika sekta mbalimbali ambazo wananchi wanaweza kuzichangamkia.

Katika hatua nyingine, Mhe. Mtambi ameagiza Afisa Uwagiliaji Mkoa wa Mara kutoka Tume ya Taifa ya Uwagiliaji kufika ofisini kwake Jumatatu tarehe 11 Agosti, 2025 ili kutoa taarifa ya maendeleo ya mradi wa uchimbaji wa visima saba vya uwagiliaji katika Halmashauri za Mkoa wa Mara.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Juma Chikoka amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kutoa maelekezo hayo kuhusu utoaji wa mikopo ya asilimia 10 ya Halmashauri katika Mkoa wa Mara na kuongeza kuwa miradi iwe yenye tija na inayoweza kuajiri watu wengine.

“Hizi fedha zisitolewa kwa namna ya kila mmoja apate, ni bora zitolewe kwa vikundi vichache lakini zitolewe kwa malengo makubwa ya kuinua uchumi wa wanavikundi na kutoa ajira katika jamii” amesema Mhe. Chikoka.

Mhe. Chikoka amesema hata kiwango cha fedha kinachotolewa katika vikundi kiboreshwe ili kikundi kinachopata fedha hizo kiweze kutekeleza mradi mkubwa wenye ubunifu, tija na ambao utakuwa na maendeleo endelevu.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Mara Mhandisi Vedastus Maribe amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuwahamasisha na kusajiri vikundi vya wanawake, wenye ulemavu na vijana katika vikundi vya kutoa huduma, ukandarasi na uwakala nakadhalika ili viweze kupewa zabuni na taasisi nunuzi.

“Sisi taasisi nunuzi tunatakiw akutoa asilimia 30 ya zabuni kwa vikundi hivyo katika manunuzi yetu kwa mwaka lakini Mkoa wa Mara hauna vikundi kama hivyo vilivyosajiriwa na Halmashauri na kwa hivyo havinufaiki na fursa hizo” amesema Mhandisi Maribe.

Mhandisi Maribe amewataka Maafisa Maendeleo ya Jamii kuwahamasisha wananchi waliopo katika makundi maalum katika jamii kujiunga katika vikundi vya utoaji huduma na uzalishaji mali ili kuweza kunufaika na zabuni mbalimbali za manunuzi zinazotangazwa na taasisi nunuzi.

Halmashauri hapa nchini zinatakiwa kutoa asilimia 10 ya mapato ya ndani kwa ajili ya kuwapa mikopo isiyo na riba vikundi vya wanawake, watu wenye ulemavu na vijana ili kufanikisha biashara za vikundi hivyo.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kanali Mtambi ateta na viongozi wa NHIF

    August 05, 2025
  • Mtambi ataka maboresho utoaji wa mikopo ya asilimia 10

    August 06, 2025
  • Mtambi ataka Hamasa Mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 06, 2025
  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa