• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kanali Mtambi ateta na viongozi wa NHIF

Posted on: August 5th, 2025

Adeladius Makwega-Musoma MARA.

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 05 Agosti, 2025 amewapokea na kufanya mazungumzo na viongozi wa Mfuko wa Bima ya Afya ya Taifa (NHIF) na kutaka kuhakikisha huduma za Madaktari Bingwa zinafika vijijini maana vipo Vituo vya Afya vyenye vifaa vinavyoweza kutumiwa na mabingwa hao kuwapa huduma Watanzania.

“Madaktari bingwa na bobezi kwa sasa wanaweza kuruhusiwa kutibu maeneo ya vijijini kwa kuwa mazingira yanaruhusu baada ya Serikali kuwekeza katika ujenzi wa Vituo vya Afya katika maeneo mbalimbali hapa nchini” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amesema utoaji wa huduma za kibingwa maeneo ya vijijini utasaidia kuwapunguzia safari baadhi ya wagonjwa wanaopewa rufaa na kwenda mbali kwa ajili ya matibbu ya kibingwa.

Kanali Mtambi katika mazungumzo hayo ametoa hoja sita ambazo aliomba Wizara Afya na NHIF kuzifanyia kazi ikiwamo pia mifumo ya NHIF kusomana, makundi maalumu kupewa huduma vizuri na kuzitatua changamoto zote kwa wakati.

Akizungumza katika mapokezi hayo, Mkurugenzi Mkuu wa NHIF Dkt. Irene Isaka amesema NHIF imeshapokea mapendekezo hayo kutoka ngazi mbalimbali ikiwamo Wizara husika suala hilo litafanyiwa kazi ili kuhakikisha Mtanzania anahudumiwa vizuri kwa ngazi yoyote anayokwenda kutibiwa.

“Sisi kama NHIF tunashukuru sana, maana mazungumzo haya yametupa picha kuwa Kanali Mtambi unafahamu kile kinachofanywa na NHIF na kile kinachofanywa na Wizara ya Afya, tumepata matumaini kuwa Bima ya Afya kwa Wote sheria ipo tayari na Kanali Mtambi wewe ni Balozi wetu” amesema Dkt. Isaka.

Dkt. Isaka amesema wametembelea Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara kwa lengo la kuweka uelewa wa pamoja baina ya mfuko huu na uongozi wa Mkoa wa Mara, maana mara nyingi mikoa ndiyo inayofanya kazi na wananchi moja kwa moja katika utekelezaji wa shughuli za kila siku.

Katika kikao hicho, Dkt. Isaka aliambatana na baadhi ya wajumbe wa Bodi ya NHIF wakiongozwa na Bi Zubeda Chande ambaye ni Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya NHIF pamoja na maafisa wengine.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kanali Mtambi ateta na viongozi wa NHIF

    August 05, 2025
  • Mtambi ataka maboresho utoaji wa mikopo ya asilimia 10

    August 06, 2025
  • Mtambi ataka Hamasa Mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 06, 2025
  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa