• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi ataka Hamasa Mbio za Mwenge wa Uhuru

Posted on: August 6th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 06 Agosti, 2025 ameongoza kikao cha pili cha Kamati ya Mkoa ya mbio za Mwenge wa Uhuru, 2025 kwa ajili ya kujadili maandalizi na maagizo yaliyotolewa na kuzitaka Wilaya kuweka mkakati maalum wa kuhakikisha hamasa ya wananchi katika mbio za Mwenge wa Uhuru. 

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Mtambi amezitaka Kamati za Usalama za Wilaya kuhakikisha wananchi wanapata hamasa ya kutosha ili waweze kujitotokeza kwa wingi kushiriki mapokezi, ukaguzi wa miradi na mikesha ya Mwenge wa Uhuru.

“Mbio za Mwenge wa Uhuru zinahitaji ushiriki wa watu, hivyo Kamati za Usalama za Wilaya ziweke mkakati wa kufanya amsha amsha katika katika maeneo yote yatakayopitiwa na Mbio za Mwenge wa Uhuru katika maeneo yao” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amewataka viongozi na watendaji kuangalia namna bora ya kufunika mambo yote yanayoendelea katika jamii na kuamsha hamasa itakayowawezesha wananchi wengi kushiriki mbio, mapokezi na mkesha wa Mwenge wa Uhuru katika maeneo yao.

Aidha, Mhe. Mtambi amewataka Wakuu wa Wilaya kusimamia maboresho yote yanayohitajika katika miradi itakayopitiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 na kutoa taarifa ya utekelezaji wa maagizo ya kikao hicho siku ya jumatatu tarehe 11 Agosti, 2025.

Kanali Mtambi amewataka Wakurugenzi wa Halmashauri kutumia mwongozo wa miradi ya Mwenge katika utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo inayoendelea katika maeneo yao ili kuhakikisha utekelezaji wa miradi hiyo unakidhi viwango vya ubora na nyaraka za miradi zinatunzwa vizuri.

Mhe. Mtambi amemtaka Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara kufuatilia kwa ukaribu maandalizi ya tukio la Mwenge wa Uhuru kuwasha Mwenge wa Mwitongo litakalofanyika nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere tarehe 18 Agosti, 2025 wakati Mwenge wa Uhuru ukiendelea na mbio zake katika Wilaya ya Butiama.

Kwa upande wake, Katibu wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara Ndugu Iddi Mkowa amepongeza maandalizi ya Mbio za Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Mara mpaka sasa na kuwataka viongozi na watendaji kukamilisha maagizo yaliyotolewa na kikao kuhusiana na miradi hiyo.

Ndugu Mkowa amekihakikishia kikao hicho kuwa CCM Mkoa wa Mara itashiriki kikamilifu katika maeneo yote na wanaendelea kuwahamasisha wanachama wake kushiriki katika maeneo mbalimbali yatakayofikiwa na mbio za Mwenge wa Uhuru kwa mwaka 2025.

Bwana Mkowa amewapongeza watendaji wote wanaosimamia shughuli za maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 kwa kazi nzuri waliyoifanya katika katika maandalizi hayo. 

Kwa upande wake, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Ndugu Gerald Musabila Kusaya amewashukuru wadau mbalimbali waliochangia shughuli za mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2025 katika Mkoa wa Mara na kuwakumbusha wadau walioombwa michango mbalimbali kuchangia kama walivyoombwa.

“Ninaomba kutumia fursa hii kuushukuru sana Mgodi wa Dhahabu wa Barrick North Mara kwa kuchangia mafuta ya magari ambayo yatatumika katika mbio za Mwenge wa Uhuru, 2025” amesema Ndugu Kusaya.

Awali akitoa taarifa ya maandalizi, Mratibu wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Mara Bwana Fidel Balagaye amesema maandalizi ya mbio za Mwenge wa Uhuru yanaendelea vizuri na mpaka sasa Mkoa upo katika hatua za mwisho za maandalizi. 

Bwana Balagaye amesema Mkoa unatarajia kupokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Simiyu katika Shule ya Msingi Balili, Mji wa Bunda tarehe 15 Agosti, 2025 na utakimbizwa katika Halmashauri zote za Mkoa wa Mara hadi tarehe 23 Agosti, 2025 na tarehe 24 Agosti, 2025 Mwenge utakabidhiwa katika Mkoa wa Mwanza.

“Mpaka sasa maandalizi yanaendelea vizuri na tupo mwishoni katika ukamilishaji, niwaombe wananchi kujitokeza kwa wingi kuupokea na kuushangilia Mwenge wa Uhuru katika Mkoa wa Mara”, amesema Bwana Balagaye.

Kikao hicho kimehudhuriwa na Kamati ya Usalama ya Mkoa, Wakuu wa Wilaya, viongozi wa CCM Mkoa wa Mara, Menejimenti na baadhi ya maafisa wa Sekretarieti ya Mkoa wa Mara, wakuu wa taasisi za umma, Wakurugenzi wa Halmashauri na baadhi ya maafisa wa Halmashauri, pamoja na wadau wa Mbio za Mwenge Mkoa wa Mara. 

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kanali Mtambi ateta na viongozi wa NHIF

    August 05, 2025
  • Mtambi ataka maboresho utoaji wa mikopo ya asilimia 10

    August 06, 2025
  • Mtambi ataka Hamasa Mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 06, 2025
  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa