• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Watoto 481,104 kupata chanjo Mara

Posted on: February 15th, 2024

Jumla ya watoto 481,104 wenye umri wa miezi tisa hadi miaka mitano wanatarajiwa kupatiwa chanjo ya magonjwa ya Surua na Rubella katika Mkoa wa Mara kuanzia leo tarehe  15 Februari, 2024 hadi tarehe 18 Februari, 2024.

Akizindua zoezi la utoaji wa chanjo hiyo katika Kituo cha Afya Nyasho, Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Said Mohamed Mtanda amesema chanjo hiyo ni salama na  muhimu sana kwa watoto na amewapongeza wazazi na walezo na waliojitokeza kuwaleta watoto kupata chanjo.

“Ninawapongeza zaidi akina Baba ambao wamefika hapa kwa ajili ya kuleta watoto kupata chanjo kwa kuonyesha mfano mzuri katika jamii kwa kuzingatia mambo muhimu katika malezi ya watoto, ikiwemo chanjo” amesema Mhe. Mtanda.

Mhe. Mtanda amewataka wananchi kuhakikisha watoto wote wenye umri wa kupata chanjo hiyo wanapata na kuzingatia ushauri unaotolewa na wataalamu wa afya kuhusu chanjo na masuala ya afya kwa ujumla kwani mtoto asiyepata chanjo zote ni hatari kwa afya yake na afya ya wengine wanaomzunguka.

Mhe. Mtanda ameeleza kuwa kama kauli mbiu inavyosema “onesha upendo mpeleke mtoto akachanje”amewataka wazazi, walezi na jamii kuonyesha upendo wao kwa watoto kwa kuhakikisha wanapata chanjo hii muhimu.  

Mkuu wa Mkoa amewataka viongozi wa ngazi za vijiji, Kata, Tarafa na Wilaya kutoa ushirikiano kwa wataalamu wa Sekta ya Afya ili kuweza kufanikisha zoezi la chanjo katika Mkoa wa Mara.

Wakati huo huo, Mkuu wa Mkoa amewapongeza watumishi wa Kituo cha Afya Nyasho, Manispaa ya Musoma kwa kazi yanayoifanya katika kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa ikilinganishwa na idadi ya watumishi waliopo katika kituo hicho.

Mhe. Mtanda amewataka kuendelea kutoa huduma wakati Serikali inaendelea kukarabati na kuboresha Hospitali ya Manispaa ya Musoma ambayo inatarajiwa kupunguza idadi ya wagonjwa wanaotibiwa katika Kituo cha Afya Nyasho.   

Akizungumza katika uzinduzi huo, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Dkt. Khalfani Haule ameeleza kuwa Wilaya ya Musoma inatarajia kutoa chanjo kwa watoto 86,000 ambapo kati ya watoto hao Manispaa ya Musoma inatarajiwa kuchanja watoto 29,000 na Halmashauri ya Wilaya ya Musoma inatarajia kuchanja watoto 57, 000.

Dkt. Haule amemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuchagua kuzindua chanjo hiyo Kimkoa katika Wilaya ya Musoma na kwa kutenga muda na kushiriki katika uzinduzi huo.

 Uzinduzi huo umehudhuriwa na Kaimu Katibu Tawala Mkoa wa Mara Dkt. Zabron Masatu; Meya wa Manispaa ya Musoma Mhe. William Gumbo, mwakilishi kutoka Wizara ya Afya, watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara na  watumishi wa Manispaa ya Musoma.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kanali Mtambi ateta na viongozi wa NHIF

    August 05, 2025
  • Mtambi ataka maboresho utoaji wa mikopo ya asilimia 10

    August 06, 2025
  • Mtambi ataka Hamasa Mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 06, 2025
  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa