• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Uwanja wa Ndege Musoma kukamilika Septemba, 2025

Posted on: April 13th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 11 Aprili, 2025 ametembelea mradi wa ukarabati na upanuzi wa Uwanja wa Ndege Musoma uliopo katika Kata ya Mkendo, Manispaa ya Musoma na kuzitaka taasisi zote zinazohusika na mradi huo kuhakikisha unakamilika kabla ya Septemba, 2025.

Akizungumza baada ya kupokea taarifa za maendeleo ya upanuzi na ukarabati huo, Mhe. Mtambi amesema tayari Serikali imetoa fedha za ukamilishaji wa uwanja huo na kwa kasi aliyoiona katika uwanja huo haoni sababu ya uwanja huo kutokukamilika mapema.

“Taarifa yenu na hali halisi ya utekelezaji wa mradi huu inaonyesha kuwa unaweza kukamilika kabla ya septemba, angalieni mtakachoweza kufanya ili mradi huu ukamilike mapema kutokana na umuhimu wake kwa Mkoa wa Mara” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amesema uwanja huo utakapokamilika utasaidia sana katika kuwasafirisha wananchi, watalii, madini, samaki na mizigo mingine kutoka Mkoa wa Mara kwa urahisi na haraka na utasaidia katika kukuza uchumi wa Mkoa wa Mara.

Mhe. Mtambi ameipongeza TANROADS Mkoa wa Mara kwa usimamizi mzuri wa mradi huo na kuitaka ihakikishe inakamilisha mradi huo kwa wakati na kumtaka Mkandarasi wa mradi huo kukamilisha shughuli zilizobakia ili uwanja uweze kutumika.  

Mhe. Mtambi amemtaka Meneja wa Uwanja wa Ndege Musoma kufuatilia mchakato wa ujenzi wa majengo mapya ya abiria kwa ukaribu huku akiendelea kufanya maandalizi ya kuanza kupokea ndege za abiria katika majengo ya zamani ya abiria yaliyopo katika uwanja huo. 

Kanali Mtambi amemtaka Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Juma Chikoka kufuatilia utekelezaji wa mradi huo kwa karibu na kuongeza kuwa mradi huo ukikamilika utaichangamsha sana Manispaa ya Musoma na Mkoa wa Mara kwa ujumla kibiashara na utalii.

Kwa upande wake, Meneja wa Wakala wa Barabara (TANROADS) Mkoa wa Mara Mhandisi Vedastus Maribe amesema awali mradi huo ulisimama kutokana na Mkandarasi kudai malipo yake baada ya kukamilisha sehemu ya kazi, lakini kwa sasa Mkandarasi ameshalipwa asilimia 80 ya fedha zote na anaendelea na ukamilishaji wa mradi.

“Utekelezaji wa mradi unaendelea vizuri na sasa umefikia asilimia 58 ya utekelezaji wa jumla wa mradi huu na tunatarajia kuukamilisha mwezi Septemba, mwaka huu” amesema Mhandisi Maribe.

Mhandisi Maribe amesema wananchi wote waliotakiwa kulipwa fidia ili kupisha mradi wameshalipwa na wanaendelea na maandalizi ya kuhama katika eneo hilo ili upanuzi wa uwanja huo uweze kuendelea.  

Kwa upande wake, Meneja wa Uwanja wa Ndege Musoma kutoka Mamlaka ya Viwanja vya Ndege Tanzania (TAA) Frank Msofe amesema taratibu za kukarabati na kuweka sawa majengo yaliyopo kwa ajili ya kutumika kupokea abiria zinaendelea wakati wakisubiria ujenzi wa majengo ya kisasa ya abiria katika uwanja huo.

Bwana Msofe amesema tayari Serikali imeanza mchakato wa kuwalipa wananchi 58 fidia ya zaidi ya shilingi bilioni tano kwa ajili ya kupisha ujenzi wa majengo ya kisasa ya kupokelea abiria katika uwanja huo.

Bwana Msofe amesema baada ya wananchi kulipwa fidia hizo, TAA itajenga majengo ya kisasa ya abiria katika uwanja huo ili abiria watakaotumia uwanja huo waweze kuhudumiwa vizuri zaidi.  

 Katika ziara hiyo, Mhe. Mtambi ameambatana na Mkuu wa Wilaya ya Musoma, Maafisa kutoka Sekretarieti ya Mkoa wa Mara, TANROADS, TAA, na Wakandarasi na wazabuni wanaotekeleza miradi huo.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kanali Mtambi ateta na viongozi wa NHIF

    August 05, 2025
  • Mtambi ataka maboresho utoaji wa mikopo ya asilimia 10

    August 06, 2025
  • Mtambi ataka Hamasa Mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 06, 2025
  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa