• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Rwezimula ataka mabadiliko baada ya mafunzo

Posted on: February 20th, 2024

Naibu Katibu Mkuu –Elimu, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Dkt. Franklin Rwezimula leo amefungua awamu ya kwanza ya mafunzo  ya kuwajengea uwezo wa uongozi, usimamizi na uendeshaji wa shule za msingi Walimu Wakuu wa Shule za Msingi za Mkoa wa Simiyu yanayofadhiliwa na Mradi wa BOOST na kusimamiwa na Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM).

Akizungumza katika ufungaji wa mafunzo hayo, Dkt. Rwezimula amewataka walimu hao kufuatilia kikamilifu mafunzo hayo na kwenda kubadilisha utendaji kazi katika vituo vyao vya kazi ili kuboresha elimu ya msingi hapa nchini.

“Ni matumaini yangu kuwa mafunzo haya yatawawezesha kusimamia shule kwa ufanisi hasa wakati huu tunapoanza kutekeleza mitaala mipya iliyoanza kutumika mwaka huu kwa wanafunzi wa darasa la kwanza hadi la tatu” amesema Dkt. Rwezimula.

Dkt. Rwezimula amewataka Wakuu wa Shule kuongoza shule kwa kufuata sheria na taratibu za utumishi wa umma na kusimamia miradi ya elimu wanayotakiwa kusimamia kwa ufanisi.

Dkt. Rwezimula ameupongeza uongozi wa ADEM kwa kuendelea kutoa mafunzo ya uongozi kwa wasimamizi mbalimbali wa sekta ya Elimu hapa nchini ambayo yanaisaidia nchi katika kuboresha usimamizi wa sekta ya elimu.  

Kwa upande wake, Mratibu wa Mafunzo hayo Bwana Mashiku Thomas Ng’wandu ameeleza kuwa kwa awamu ya kwanza mafunzo hayo yamewahusisha Walimu Wakuu wa Shule za Msingi 285 kutoka Halmashauri za Bariadi, Itilima na Busega Mkoani Simiyu na yameanza tarehe 19-21 Februari, 2024.

“Lengo la mafunzo haya ni kuwajengea uwezo Walimu Wakuu katika uongozi, usimamizi na uendeshaji wa Shule za Msingi

Bwana Mashiku ameeleza kuwa awamu ya pili yatawahusisha Wakuu wa Shule 299 kutoka Halmashauri zilizobakia katika Mkoa wa Simiyu na yatafanyika Chuo cha Ualimu Bunda kuanzia tarehe 21-24 Februari, 2024.

Bwana Mashiku ameeleza kuwa katika mafunzo hayo, mahiri mbalimbali zinategemewa kuwezeshwa na wakufunzi kutoka ADEM wakishirikiana na baadhi ya wasimamizi wa elimu kutoka Mkoa wa Simiyu.

Akizungumza katika ufunguzi wa mafunzo hayo, Naibu Mtendaji Mkuu wa ADEM Dkt. Emanuel Mollel ameeleza kuwa ADEM ina wataalamu wengi waliobobea katika mafunzo ya uongozi wa elimu na ameishukuru Wizara ya Elimu kwa akuendelea kuiamini na kuwapa kazi mbalimbali.

Dkt. Mollel ameeleza kuwa miungoni mwa kazi walizopewa na Wizara hiyo ni pamoja na mafunzo kwa Maafisa Elimu wa Mikoa ambayo yanatarajiwa kufanyika hivi karibuni katika Mji wa Bagamoyo.

Akizungumzia mafunzo yanayotolewa kupitia Mradi wa BOOST Dkt. Mollel ameeleza kuwa hadi sasa ADEM imeshatoa mafunzo kwa walimu zaidi ya 6700  katika awamu ya kwanza, na katika awamu hii wanategemea kutoa mafunzo kwa walimu zaidi ya 4000 katika mikoa mbalimbali.

Dkt. Mollel amewataka walimu kutumia mafunzo hayo katika kuboresha utendaji na usimamizi wa elimu ili kuonyesha manufaa ya mafunzo hayo.

 Ufunguzi wa mafunzo hayo umehudhuriwa pia na Makaimu Katibu Tawala Wasaidizi Sehemu ya Mafunzo wa Mikoa ya Simiyu na Mara, Mwakilishi wa TAMISEMI, Mdhibiti Ubora wa Kanda ya Ziwa,  Naibu Mtendaji Mkuu wa ADEM, wakufunzi wa mafunzo hayo na baadhi ya Wakuu wa Divisheni za Elimu kutoka Mkoa wa Simiyu.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kanali Mtambi ateta na viongozi wa NHIF

    August 05, 2025
  • Mtambi ataka maboresho utoaji wa mikopo ya asilimia 10

    August 06, 2025
  • Mtambi ataka Hamasa Mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 06, 2025
  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa