• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi awahimiza viongozi wa dini kuhubiri amani

Posted on: June 11th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Evans Alfred Mtambi leo tarehe 05 Juni, 2025 akiwa ameambatana na Kamati ya Usalama ya Mkoa amezungumza na viongozi wa dini na Kamati ya Amani na Maridhiano ya Mkoa wa Mara na kuwataka kuendelea kuomba na kuhubiri amani hususan Taifa linapoelekea katika uchaguzi Mkuu.

Mhe. Mtambi amewataka viongozi wa dini kuwahamasisha waumini waweze kuchangamkia fursa zilizopo katika Mkoa wa Mara ili waweze kutafuta fedha za kufanya maendeleo yao ili kuimarisha uchumi wao na jamii kwa ujumla.  

“Jamii ikiwa na nguvu ya kiuchumi inakuwa rahisi zaidi kuihubiria suala la amani na usalama kwa kuwa hamna anayeweza kushawishika kirahisi kujiunga katika makundi yasiyofaa” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amewataka viongozi wa Dini kuuombea Mkoa wa Mara na nchi yetu Tanzania ili uchaguzi ufanyike kwa amani na utulivu na maisha ya wananchi yaendelee vizuri baada ya uchaguzi.  

Mhe. Mtambi amewataka viongozi wa Dini kukemea uvunjifu wa maadili katika jamii na kukemea mauaji ya kirejareja ya wananchi yanayotokana sababu mbalimbali ikiwemo wivu wa mapenzi na migogoro mingine katika jamii ambayo ingeweza kusuluhishwa bila kuwepo kwa mauaji hayo.

Mhe. Mtambi amewashukuru viongozi wa dini kwa kuendelea kukemea vitendo vya uvunjifu wa amani katika jamii na kwa sasa Mkoa wa Mara unafanya vizuri kulingana na takwimu zinazotolewa na Wizara ya Mambo ya Ndani inaonyesha kuwa Mkoa wa Mara haupo katika mikoa 10 inayoongoza kwa uhalifu hapa nchini.

“Mchango wenu katika kuleta haya mabadiliko ya kijamii na kuacha vitendo vya uhalifu na unyanyasaji ni mkubwa sana na kama Mkoa tunauthamini sana” amesema Mhe. Mtambi na kuongeza kuwa Dini ni chombo pekee kinachoweza kumpunguzia mtu msongo wa mawazo.

Aidha, amewataka kukemea matendo maovu kama vile mapenzi ya jinsia moja, ukeketaji na migogoro katika jamii na kuwahamasisha waumini kuishi maisha ya kindugu na mshikamano wa kijamii katika maeneo yao. 

Kikao hicho kimehudhuriwa na viongozi wa Dini, Kamati ya Usalama ya Mkoa wa Mara na baadhi ya watumishi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kanali Mtambi ateta na viongozi wa NHIF

    August 05, 2025
  • Mtambi ataka maboresho utoaji wa mikopo ya asilimia 10

    August 06, 2025
  • Mtambi ataka Hamasa Mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 06, 2025
  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa