• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi ataka Halmashari za Mara Kujifunza Bunda TC

Posted on: June 28th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo ameshiriki kikao cha Baraza la Madiwani la Halmashauri wa Mji wa Bunda na kumtaka Katibu Tawala wa Mkoa kuhakikisha Halmashauri zote za Mkoa wa Mara kwenda Halmashauri ya Mji wa Bunda kujifunza namna ya kujibu hoja za ukaguzi za Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali (CAG).

“Ninatoa muda mfupi Halmashauri zote za Mkoa wa Mara zije kujifunza hapa namna ya kujibu hoja za ukaguzi ili zikaboresha taarifa zao na za utekelezaji wa hoja za ukaguzi na maelekezo ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali za Mitaa (LAAC)” amesema Mhe. Mtambi.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Mtambi pia ameipongeza Halmashauri kwa kupata hati safi ya ukaguzi kwa miaka minne mfululizo na kuwa na hoja chache za ukaguzi baada ya kufanikiwa kufunga hoja nyingi zilizokuwa zimehojiwa na CAG hapo awali.

Mhe. Mtambi ameipongeza Halmashauri hiyo kwa makusanyo ya mapato ya ndani ambapo hadi kufikia tarehe 31 Mei, 2024 Halmashauri hiyo ilikuwa imekusanya shilingi 1,879,551,750 kati ya lengo la kukusanya shilingi  2, 058,480,000 kwa mwaka wa fedha 2023/2024.

Mhe. Mtambi amesema makusanyo hayo ni sawa na asilimia 91.3 ya fedha yote iliyopangwa kukusanywa  na kuongeza kuwa ni matumaini yake watafikia malengo ya makusanyo hadi kufikia tarehe 30 Juni, 2024.

Mhe. Mtambi ameitaka Halmashauri hiyo kuandaa mpango kazi na kusimamia utekelezaji wa kujibu hoja za ukaguzi na maagizo ya Kamati ya Bunge ya Hesabu za Serikali (LAAC) kwa wakati.

Mhe. Mtambi ameitaka Halmashauri kutumia Mfumo wa Taifa wa Manunuzi (NEST) katika kufanya manunuzi na kufanya mafunzo kwa watumishi na Madiwani kuhusu mfumo wa NEST, sheria ya manunuzi ya mwaka 2023 na kanuni zake.

Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Wilaya ya Bunda Mhe.Mayaya Abraham Magese amempongeza Mkuu wa Mkoa kwa kazi nzuri anayoifanya tangu alipoingia Mkoa wa Mara na hususan katika ukaguzi wa miradi ya maendeleo na ufuatiliaji wa utendaji wa watumishi.  

Amemshukuru Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Bunda Mhe. Michael Kweka na Baraza la Madiwani la Halmashauri ya Mji wa Bunda kwa kazi nzuri wanayoifanya katika kusimamia Halmashauri hiyo katika utendaji wake.

Mheshimiwa Magese ametolea mfano wa hoja za CAG ambapo Halmashauri hiyo katika ukaguzi wa mwaka 2022/2023 ilipata hoja 21 na hadi sasa imefanikiwa  kufuta hoja 13 na sasa imebakiza hoja nane tu na sehemu kubwa ya hizi hoja zipo nje ya uwezo wao.

Mheshimiwa   Magese amesema huwa Halmashauri hii wanafanya kazi vizuri na Chama cha Mapinduzi Wilaya ya Bunda hakina wasiwasi na usimamizi wao wa miradi na utoaji wa huduma kwa wnaanchi.

Katika ukaguzi wa mwaka wa fedha 2022/2023 Halmashauri ya Mji wa Bunda ulipata hoja 21 na kati ya hoja hizo, hoja 13 zimehakikiwa na kufungwa na kwa sasa bado hoja 8 ambazo zipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji.

Aidha, Halmashauri hiyo ilikuwa na hoja za miaka ya nyuma 38 na kati ya hoja hizo, hoja 24 zilihakikiwa na kufungwa, hoja 11 zipo kwenye hatua za utekelezaji, hoja 2 zimejirudia na hoja 1 imepitwa na wakati.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kanali Mtambi ateta na viongozi wa NHIF

    August 05, 2025
  • Mtambi ataka maboresho utoaji wa mikopo ya asilimia 10

    August 06, 2025
  • Mtambi ataka Hamasa Mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 06, 2025
  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa