• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mtambi aipongeza Manispaa ya musoma kwa hati safi miaka mitano mfululizo

Posted on: June 11th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi ameshiriki Baraza Maalum la Madiwani linalojadili hoja za Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Hesabu za Serikali katika Manispaa ya Musoma na kuipongeza Manispaa hiyo kwa kupata hati safi kwa miaka mitano mfululizo.

Akizungumza katika kikao hicho, Mhe. Mtambi amelipongeza Baraza la Madiwani, Menejimenti, watumishi wa Manispaa hiyo na wadau wote waliohusika katika kuiwezesha Manispaa kupata hati safi ya ukaguzi.

“Hii inaonyesha Manispaa ina uimara wa mifumo ya usimamizi wa mapato na matumizi ya Manispaa na juhudi za kila mmoja katika utekelezaji wa majukumu” amesema Mhe. Mtambi.

Mhe. Mtambi amelitaka Baraza la Madiwani kusimamia kasoro za usimamizi wa mikataba na manunuzi ili thamani ya fedha katika miradi iweze kuonekana na kuhakikisha manunuzi yote yanafanyika kupitia mfumo wa ununuzi na kupunguza hoja za ukaguzi katika Manispaa hiyo. 

Kanali Mtambi ameiagiza Halmashauri ya Manispaa ya Musoma kuandaa mkakati wa kumaliza hoja za ukaguzi na maagizo ya LAAC na kuuwasilisha ofisini kwake tarehe 30 Juni, 2025 na kuhakikisha maafisa wanaosababisha hoja wanachukuliwa hatua za kiutumishi.

Mhe. Mtambi ametoa wiki mbili kwa Katibu Tawala Mkoa wa Mara kumrejesha Bashiri Gasori aliyekuwa Afisa Uvuvi wa Manispaa hiyo na baadaye kuhamia Manispaa ya Ilemela baada ya kubainika kuwa uhamisho wake haukuwa halali.

Mhe. Mtambi amesema hali ya ukusanyaji wa mapato katika Manispaa ya Musoma hairidhishi na kuitaka kuweka mikakati ya kuongeza vyanzo vya mapato na kukusanya mapato kwa ufanisi ili kupata fedha za kuiendesha Halmashauri na kutekeleza miradi ya maendeleo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Wilaya ya Musoma Mhe. Juma Chikoka amesema hoja nyingi za Halmashauri hiyo zilipaswa kuwa zimefungwa kwa sababu majibu ya hoja nyingi kati ya hizo yapo wazi na ndani ya uwezo wa Manispaa kujibu.

Mhe. Chikoka amesema Manispaa hiyo itaandaa utaratibu wa kuwatambua ni maafisa gani wanaowasababishia hoja za ukaguzi watawachukulia hatua na kuwataka watumishi kila mtu atimize wajibu wake. 

Mhe. Chikoka amesema Wilaya ya Musoma itasimamia uandaaji wa mkakati wa kukamilisha hoja za ukaguzi na itahakikisha Manispaa inawasilisha mkakati huo kabla ya tarehe 30 Juni, 2025 na inafunga hoja nyingi ambazo majibu yake yamo ndani ya uwezo wa Manispaa. 

Kwa upande wake, Mwekahazina wa Manispaa ya Musoma ACPA Emmanuel Abraham amesema katika mwaka wa fedha 2023/2024 Halmashauri ilikuwa na hoja 72 na baada ya uhakiki hoja 37 zimefungwa huku hoja nyingine 48 zikiendelea kufayiwa kazi.

Aidha, Bwana Abraham amesema Manispaa ilikuwa na maagizo saba ya Kamati ya Bunge ya Fedha za Serikali za Mitaa (LAAC) ambapo maagizo mawili yamefungwa na maagizo matano yanaendelea kufanyiwa kazi.

Bwana Abraham amesema pamoja na HAlmashauri hiyo kupata changamoto ya kufunga hesabu katika mfumo wa uhasibu serikalini (MUSE) lakini baada ya hesabu hizo kufungwa imepata hati safi ya ukaguzi.

Kikao hicho kilihudhuriwa na Katibu Tawala Mkoa wa Mara, Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Musoma, Maafisa kutoka ofisi za ukaguzi na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, madiwani na menejimenti ya Manispaa ya Musoma.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kanali Mtambi ateta na viongozi wa NHIF

    August 05, 2025
  • Mtambi ataka maboresho utoaji wa mikopo ya asilimia 10

    August 06, 2025
  • Mtambi ataka Hamasa Mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 06, 2025
  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa