• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Miradi ya TACTIC kuboresha muonekano wa Musoma

Posted on: August 12th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo tarehe 12 Agosti 2025 amekuwa mgeni rasmi katika hafla ya utiaji saini ujenzi wa Miradi ya Uboreshaji wa Miji Tanzania (TACTIC) katika Manispaa ya Musoma itakayogharimu shilingi bilioni 19.975.

Akizungumza katika hafla hiyo, Mhe. Mtambi amesema miradi hiyo inayotekelezwa katika Miji 45 hapa nchini inadhaminiwa na Benki ya Dunia na itakapokamilika itabadilisha  mandhari ya Manispaa ya Musoma.

“Binafsi nina furaha kubwa, maana ujenzi wa miradi hii ikiwamo Soko la Nyasho, barabara za ndani ya Manispaa na Stendi ya Bweri itasadia kubadilisha muonekano wa Manispaa ya Musoma” amesema Kanali Mtambi.

Mhe. Mtambi amesema miradi hii itakapokamilika italeta mabadiliko chanya kwa wananchi na wageni katika Manispaa ya Musoma na kuboresha mazingira ya biashara na kupandisha thamani ya maeneo husika itapanda na kuongeza mapato ya Manispaa ya Musoma.

Mhe. Mtambi amewataka viongozi na wataalamu kuisimamia vizuri miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na kwa ubora na kumtaka mkandarasi wa miradi hiyo MS Henan Highway Engineering Group Company Limited kutekeleza mradi huo kwa ubora na kwa wakati kulingana na mkataba.

Awali akitoa taarifa ya mradi huo, Mkurugenzi wa Manispaa ya Musoma Ndugu Bosco Nduguru amesema mradi hiyo inatarajiwa kutekelezwa kwa muda wa miezi 15 kuanzia tarehe 15 Agosti, 2025 hadi Novemba, 2026 na itahusisha ujenzi wa miradi mikubwa mitatu pamoja na ofisi za usimamizi na uratibu wa ujenzi wa miradi hiyo.

Ndugu Ndunguru amesema miradi itakayojengwa katika Manispaa ya Musoma kupitia mradi wa TACTIC ni pamoja na barabara tatu za Mukendo, Shaabani na Musoma Bus –Saanane; Soko la Nyasho na Stendi ya Bweri.   

Hafla hiyo imehudhuriwa na Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara, Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia miundombinu kutoka Ofisi ya Rais- TAMISEMI, Kamati ya Usalama ya Wilaya ya Musoma, viongozi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Mara, watumishi kutoka Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara, Halmashauri ya Manispaa ya Musoma na Mkandarasi wa miradi hiyo. 

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Mwenge wa Uhuru kupitia miradi ya bilioni 26.6 Mara

    August 13, 2025
  • Miradi ya TACTIC kuboresha muonekano wa Musoma

    August 12, 2025
  • Kanali Mtambi ateta na viongozi wa NHIF

    August 05, 2025
  • Mtambi ataka maboresho utoaji wa mikopo ya asilimia 10

    August 06, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa