• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Mara Yaitaka TBA kukamilisha jengo la Halmashauri ya Mji wa Tarime

Posted on: July 26th, 2021

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Ally Salum Hapi ameitaka Wakala wa Majengo Tanzania (TBA) kukamilisha ujenzi wa jengo la Halmashauri ya Mji wa Tarime kulingana na muda uliopo katika mkataba wao.

Mheshimiwa Hapi ametoa maagizo hayo leo tarehe 23 Julai 2021 wakati Kamati ya Siasa ya Chama cha Mapinduzi katika Mkoa wa Mara ilipotembelea mradi huo.

“Huu mradi umechelewa sana bila sababu za msingi, sasa nataka tarehe 28 Septemba 2021 mradi huu uwe umekamilika na uanze kutumika na hakutakuwa na nyongeza tena ya muda wa utekelezaji wa mradi huu” ameagiza Mheshimiwa Hapi.

Ameitaka TBA baada ya siku tatu kufunga taa katika eneo hilo na kuanza kutekeleza mradi huo usiku na mchana ili uweze kukamilika kwa wakati na kumtaka Mkuu wa Wilaya ya Tarime kusimamia utekelezaji wa agizo hilo.

Aidha mamemtaka msimamizi wa mradi huo kusafisha mazingira ya maradi huo “Na sitaki kukuta site chafu namna hii nikija tena” alisema Mheshimiwa Hapi.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mara Mheshimiwa Samweli Kiboye amesema kuwa TBA wanatabia ya kuchelewesha miradi

“Ningekuwa mimi ndio ninatoa tenda nisingekuwa ninawapatia tenda TBA, hawa wakishachukua pesa wanapotea na wakisikia tunakuja kukagua wanarudi kwenye mradi” alisema Mheshimiwa Kiboye.

Mheshimiwa Kiboye ameeleza kuwa mradi huo wameukataa kwa sababu unatekelezwa kwa muda mrefu mmno bila sababu za msingi.

Kwa upande wake Msimamizi wa Mradi huo kwa upande wa TBA Mhandisi Mohammed Mohammed ameeleza kuwa mkataba wa ujenzi  wa jengo hilo ni bilioni 3.1 na kati ya hizo TBA tayari wameshalipwa shilingi bilioni 2.1.

“Kazi zinazoendelea katika eneo hili ni ufyatuaji wa matofali kwa ajili ya kujenga kuta za jengo hili na kwa mujibu wa mkataba tunatarajia kukamilisha ifikapo tarehe 28 Septemba 2021”alisema Mhandisi Mohammed.

Ameeleza kuwa mradi huo ulianza kutekelezwa mwaka 2017 na baadaye ulisimamishwa na serikali na kuanza tena baada ya muda.

Kamati ya Siasa ikiwa katika Wilaya ya Tarime ilitembelea  Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Tarime na mradi wa jengo la ofisi za Halmashauri ya Mji wa Tarime.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kanali Mtambi ateta na viongozi wa NHIF

    August 05, 2025
  • Mtambi ataka maboresho utoaji wa mikopo ya asilimia 10

    August 06, 2025
  • Mtambi ataka Hamasa Mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 06, 2025
  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa