• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

Kanali Mtambi akabidhiwa ofisi Mara

Posted on: April 9th, 2024

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza Mhe. Said Mohamed Mtanda leo amekabidhi ofisi kwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi katika hafla fupi iliyofanyika katika Ukumbi wa Uwekezaji, Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Akizungumza katika hafla hiyo, Kanali Mtambi amewataka viongozi na watumishi wa umma wa Mkoa wa Mara kutimiza wajibu wao kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za uongozi na utumishi wa umma na kuweka kipaumbele katika kuwahudumia wananchi.

“Lengo ni kuhakikisha kuwa tunatimiza wajibu wetu wa kuwatumikia wananchi na kutatua changamoto zao kwa nafasi zetu tulizonazo, sitavumilia uzembe wa aina yoyote na kutoka kwa mtu yoyote” amesema Mhe. Kanali Mtambi.

Aidha, amezitaka taasisi zinazotakiwa kutoa huduma saa 24 kwa siku kuhakikisha zinatoa huduma kikamilifu muda wote ikiwemo hospitali, jeshi na polisi kuhakikisha wanaboresha pia huduma zinazotolewa usiku na siku za mwishoni mwa wiki.

“Kuna hii tabia ukienda hospitali usiku au siku za mwisho wa wiki unaambiwa huwezi kupata vipimo au mtaalamu Fulani hayupo mgonjwa anaambiwa njoo siku nyingine, hili halikubaliki Mkoa wa Mara” amesema Mhe. Mtambi.

Amezitaka Mamlaka za Serikali za Mitaa kufuata sheria, taratibu na kanuni katika kutekeleza miradi ya maendeleo ili iweze itekelezwe kwa ubora na ikamilike kwa wakati unaotegemewa ili wananchi wapate huduma katika miradi hiyo.

Mhe. Mtambi amesema anataka kupunguza uhalifu katika Mkoa wa Mara na kumtaka Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mara kuwashughulikia wahalifu kabla hawajafanya uhalifu na kumtaka kufufua mifumo  ya kiintelijensia ifanye kazi ya kubaini uhalifu kabla haujatokea.

Amemwagiza Mkuu wa Wilaya ya Musoma kuhakikisha mlipuko wa kuharisha na kutapika ulioanza katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma unadhibitiwa na hauenei katika Mkoa wa Mara na kufanya ukaguzi wa usafi wa mazingira mara kwa mara.

Amewaagiza mameneja wa Mkoa wa Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) na Wakala wa Barabara za Mijini na Vijijini (TARURA) kuhakikisha kuwa barabara na madaraja yote yanapitika muda wote pamoja na  mvua zinazoendelea kunyesha.

Amezitaka Mamlaka na wakala za Maji katika Mkoa wa Mara kuhakikisha huduma ya maji inapatikana kwa wananchi na miradi ya maji inakamilika kwa wakati na kutoa huduma kwa wananchi ili kuwawezesha wananchi kufanya shughuli nyingine za maendeleo.

Kwa upande wake, Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, Mhe. Said Mohamed Mtamba amewashukuru viongozi,  watumishi na wananchi wa Mkoa wa Mara kwa ushirikiano mkubwa waliompatia wakati wote akiwa Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Mhe. Mtanda ameeleza kuwa pamoja na mambo mengine yanayosikika kuhusu Mkoa wa Mara kwa watanzania wengine, wananchi wa Mkoa wa Mara ni watu wema, wakarimu na wanapenda maendeleo yao.

Mhe. Mtanda amempongeza Mhe. Mtambi kwa kuaminiwa na kuteuliwa kuuongoza Mkoa wa Mara na kuwataka watu wa Mkoa wa Mara kumpa ushirikiano ili aweze kutekeleza majukumu yake kikamilifu.  

Hafla ya makabidhiano imehudhuriwa na viongozi wa dini, viongozi wa vyama vya siasa, Wakuu wa Wilaya, Kamati ya Usalama ya Mkoa, Meya wa Manispaa ya Musoma, Wakuu wa Sehemu na Vitengo vya Sekretarieti ya Mkoa wa Mara, Makatibu Tawala wa Wilaya, Wakurugenzi wa Halmashauri, wakuu wa taasisi za umma, wafanyakazi wa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kanali Mtambi ateta na viongozi wa NHIF

    August 05, 2025
  • Mtambi ataka maboresho utoaji wa mikopo ya asilimia 10

    August 06, 2025
  • Mtambi ataka Hamasa Mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 06, 2025
  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa