• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua pepe |
MARA REGION

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mkoa wa Mara

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhamira
    • Misingi Mikuu
  • Utawala
    • Muundo wa Uongozi
    • Seksheni
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Vitengo
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • Wilaya
    • Wilaya ya Musoma
    • Wilaya ya Butiama
    • Wilaya ya Bunda
    • Wilaya ya Rorya
    • Wilaya ya Tarime
    • Wilaya ya Serengeti
  • Halmashauri
    • Manispaa ya Musoma
    • Bunda DC
    • Bunda Mji
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Mji
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Fursa za Uwekezaji
  • Huduma
    • Maji
    • Elimu
    • Afya
    • Miundombinu
    • TEHAMA
  • Machapisho
    • Miongozo
    • Utaratibu
    • Ripoti
    • Sera
    • Fomu ya Maombi
    • Fomu ya Ahadi ya Uadilifu
    • Mkataba wa Huduma kwa Mteja
  • Kituo cha Habari
    • Taarifa kwa Vyomba vya Habari
    • Video
    • Hotuba
    • Maktaba ya Picha
    • Habari
    • Matukio

HHAPI: Viongozi na Watumishi tutimize wajibu wetu kwa Wananchi

Posted on: June 22nd, 2021

HAPI: VIONGOZI NA WATUMISHI TUTIMIZE WAJIBU WETU KWA WANANCHI

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Ally Salum Hapi amewataka viongozi na watumishi wa serikali katika Mkoa wa Mara kutimiza wajibu wao kikamilifu ili kuweza kuleta maendeleo yanayotarajiwa kwa wananchi wa Mara.

Mheshimiwa Hapi ametoa kauli hiyo leo katika maeneo mbalimbali baada ya kuwasili na kupokelewa na viongozi mbalimbali wa serikali, Chama cha Mapinduzi, vyombo vya ulinzi na usalama, viongozi wa dini, watumishi wa serikali, wazee na viongozi wa mashirika na taasisi za serikali.

“Sisi wote tumetumwa na serikali kuja kuleta maendeleo na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili wananchi wa Mkoa wa Mara, kwa hiyo kila mtu kwa nafasi yake tuwajibike kutekeleza ilani ya Chama cha Mapinduzi, chama ambacho wananchi wamekichagua  kuwaletea maendeleo ” alisema Mheshimiwa Hapi. 

Amewataka viongozi na watumishi kutimiza wajibu wao bila ya kusubiri kukumbushwa wala kufuatiliwa na watu wengine ili wananchi waweze kupata manufaa wanayoyatarajia kutoka kwa serikali yao ya Chama cha Mapinduzi.  

Aidha amewataka Maafisa Utumishi ,  wakurugenzi wa halmashauri na wasimamizi wa kazi katika maeneo mbalimbali kutenga muda wa kusikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zinazowakabili  watumishi wa Mkoa wa Mara ili watumishi waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi zaidi.

Mheshimiwa Hapi amewataka viongozi na watumishi wote wa Mkoa wa Mara kushirikiana na kufanya kazi kama timu moja ambayo imeajiriwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania  ili kuweza kuleta maendeleo na kutatua changamoto za wananchi wa Mkoa wa Mara.

“Mimi ninaamini kuwa ushirikiano kati yetu viongozi na watumishi wa serikali na baina ya serikali na Chama na wadau wengine utatusaidia sana katika kutimiza wajibu wetu lakini pia katika kuwaletea wananchi maendeleo yanayohitajika kwa haraka zaidi” alisema Mheshimiwa Hapi.

Baada ya kuwasili katika Mkoa wa Mara, Mheshimiwa Hapi alipokelewa na Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mheshimiwa Mwalimu Lyidia Bupilipili, Katibu Tawala wa Mkoa wa Mara Bwana Albert Gabriel Msovela, Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Mkoa na viongozi wengine.

Mara baada ya mapokezi hayo Mheshimiwa Hapi ametembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambapo akiwa hapo amepata nafasi ya kutembelea kaburi la Baba wa Taifa,  maktaba binafsi ya Baba wa Taifa pamoja na kuzungumza na viongozi na wazee wa Wilaya ya Butiama.

Akiwa nyumbani  kwa Baba wa Taifa Mheshimiwa Hapi amepokelewa na mtoto wa Baba wa Taifa Bwana Madaraka Nyerere, wanafamilia wengine pamoja na wazee na viongozi wa Wilaya ya Butiama.

Baada ya kutoka Butiama, Mheshimiwa Hapi ametembelea  na kusaini kitabu cha wageni katika ofisi za Chama Cha Mapinduzi (CCM) Mkoa wa Mara na kupokelewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Mheshimiwa Samweli Kiboye maarufu kama Namba 3 na viongozi wengine wa CCM Mkoa wa Mara.

Baada ya hapo Mheshimiwa Hapi amezungumza na viongozi na watumishi mbalimbali wa Mkoa wa Mara waliokusanyika kumpokea katika ukumbi wa uwekezaji uliopo katika Ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mara.

Mheshimiwa Hapi amehamishiwa Mara kuchukua nafasi iliyoachwa wazi na aliyekuwa Mkuu wa Mkoa wa Mara Mheshimiwa Mhandisi Robert Gabriel Luhumbi ambaye amehamishiwa kuwa Mkuu wa Mkoa wa Mwanza baada ya Mheshimiwa Rais Samia Suluhu Hassan kufanya mabadiliko tarehe 11 Juni 2021. 

Baada ya uteuzi huo, Mheshimiwa Hapi alishiriki ziara ya Rais aliyoifanya katika Mkoa wa Mwanza akiuwakilisha Mkoa wa Mara na leo amewasili rasmi katika Mkoa wa Mara kutekeleza majukumu yake.

Matangazo ya Kawaida

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • Tazama Zote

Habari Mpya

  • Kanali Mtambi ateta na viongozi wa NHIF

    August 05, 2025
  • Mtambi ataka maboresho utoaji wa mikopo ya asilimia 10

    August 06, 2025
  • Mtambi ataka Hamasa Mbio za Mwenge wa Uhuru

    August 06, 2025
  • Kilimo cha alizeti kinga dhidi ya uvamizi wa tembo- Mtambi

    August 01, 2025
  • Tazama Zote

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
Video zaidi

Kurasa za karibu

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Tovuti Mashuhuri

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Anwani ya Posta: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Simu: +255282622305

    Simu:

    Barua pepe: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Sera ya Faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya Tovuti

Hatimiliki©2017 Mkoa wa Mara.Haki Zote Zimehifadhiwa