• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Units
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Mwenge wakagua miradi ya bilioni 6 Musoma

Posted on: August 18th, 2025

Mbio za Mwenge wa Uhuru zimeendelea katika Mkoa wa Mara ambapo katika Wilaya ya Musoma Mwenge wa Uhuru umekagua miradi yenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 6.

Ukiwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma tarehe 16 Agosti, 2025 Mwenge wa Uhuru imepitia miradi saba yenye thamani ya shilingi 2,562,794,529.18 ambayo imetekelezwa kwa michango ya  wananchi shilingi 31,927,000.00; mapato ya ndani ya Halmashauri 233,395,000.00; Serikali Kuu 1,699,192,500.00 na wahisani wa maendeleo 598,280,029.00.

Mwenge wa Uhuru katika Halmashauri ya Wilaya ya Musoma umezindua mradi wa kikundi cha vijana cha Kaburabura cha uchenjuaji wa madini, umeweka jiwe la msingi katika mradi wa maji wa Kijiji cha Muhoji; umezindua daraja la barabara ya Msinono-Kinyang’erere; na umezindua mradi wa ufugaji wa samaki kwa njia ya vizimba wa Nyamangati Agro Farm.

Aidha, Mwenge wa Uhuru umezindua ofisi za Kijiji cha Kwibara; umeweka jiwe la msingi Shule ya Sekondari Kurwaki na Kituo cha Afya Kiriba na Mkesha wa Mwenge wa Uhuru ukafanyika katika uwanja wa Shule ya Msingi Bwai.

Ukiwa katika Manispaa ya Musoma tarehe 17 Agosti, 2025, Mwenge wa Uhuru umetembelea miradi nane ya maendeleo yenye thamani ya shilingi 3,591,239,074.94 ambayo imegharimiwa na wananchi 58,400,000.00; mapato ya ndani ya Halmashauri 129,402,800.00; na Serikali kuu 3,403,436,274.93.

Miradi iliyotembelewa katika Manispaa ya Musoma ni utunzaji wa mazingira katika chanzo cha maji Bukanga- Makoko; mradi wa vizimba vya ufugaji samaki eneo la lake side; umezindua majengo matatu katika Hospitali ya Manispaa ya Musoma; na kufungua ofisi ya Mtendaji wa Mwigobero D.

Aidha, Mwenge wa Uhuru umetembelea mradi wa kikundi cha Umoja wa Mafundi Welding Nyakato-Maziwa; umeweka jiwe la msingi katika mradi wa ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami ya Mahakamu Kuu-Nyabisare; umetembelea mradi wa hifadhi ya mazingira na matumizi ya nishati safi Chuo cha Maendeleo ya Wananchi (FDC) Musoma na umeweka jiwe la msingi mradi wa Shule ya Sekondari Bubwemo.

Mkesha wa Mwenge wa Uhuru katika Manispaa ya Musoma umefanyika katika uwanja wa Shule ya Sekondari ya Mara na kwa sasa Mwenge umekabidhiwa katika Wilaya ya Butiama kuendelea na mbio zake.

Announcements

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • View All

Latest News

  • Mwenge wa Uhuru Wapitisha miradi 68 ya bilioni 26.5 Mara

    August 23, 2025
  • RC Mtambi akutana na viongozi wa dini na kuwasistiza kuhamasisha amani

    August 22, 2025
  • Wananchi Rorya wahimizwa kutumia nishati safi ya kupikia

    August 19, 2025
  • Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa awasha Mwenge wa Mwitongo kwa mara ya 61

    August 18, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.