• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Sehemu ya Mipango na Uratibu
      • Sehemu ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi
      • Sehemu ya Viwanda, Biashara na Uwekezaji
      • Sehemu ya Uratibu wa Sekta ya Uchumi na Uzalishaji
      • Sehemu ya Utawala na usimamizi wa rasilimali watu
      • Sehemu ya Huduma za Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe
      • Sehemu ya usimamizi, ufuatiliaji na ukaguzi
      • Sehemu ya Miundombinu
    • Units
      • Kitengo cha Huduma za Kisheria
      • Kitengo cha Uhasibu na Fedha
      • Kitengo cha Ukaguzi wa ndani
      • Kitengo cha Teknolojia ya Habari na Mawasiliano
      • Kitengo cha Ugavi na Manunuzi
      • Kitengo cha Maendeleo ya Jamii
      • Kitengo cha Ufuatiliaji na Tathmini
      • Kitengo cha Mawasiliano Serikalini
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Mwenge wa Uhuru kupitia miradi ya bilioni 26.6 Mara

Posted on: August 13th, 2025

Mkuu wa Mkoa wa Mara Mhe. Kanali Evans Alfred Mtambi leo ametoa taarifa kwa Waandishi wa Habari kuhusu maandalizi ya mapokezi ya Mwenge wa Uhuru na kueleza kuwa ukiwa katika Mkoa wa Mara Mwenge utapitia miradi 68 yenye thamani ya shilingi bilioni 26,547,598,285.42. 

Akizungumza katika mkutano huo uliofanyika ofisini kwake, Mhe. Mtambi amesema ukiwa katika Mkoa wa Mara, Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa Kilomita 1,123 na utatembelea na kukagua, kuweka mawe ya msingi, kufungua na kuzindua miradi 68 ya maendeleo katika Halmashauri zote tisa.

“Ninawakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Mara kushiriki mapokezi ya Mwenge wa Uhuru yatakayofanyika katika Uwanja wa Shule ya Msingi Balili, Halmashauri ya Mji wa Bunda keshokutwa kuanzia saa 12 asubuhi” amesema Mhe. Mtambi.  

Mhe. Mtambi amesema Mkoa wa Mara utapokea Mwenge wa Uhuru kutoka Mkoa wa Simiyu tarehe 15 Agosti, 2025 katika Halmashauri ya Mji Bunda na kuukimbiza katika Halmashauri hadi tarehe 23 Agosti, 2025 na baadaye kuukabidhi Mwenge wa Uhuru Mkoa wa Mwanza tarehe 24 Agosti, 2025.

Kanali Mtambi ameitaja ratiba ya Mwenge wa Uhuru kuwa inanza tarehe 15 Agosti, 2025 ambapo Mwenge utakimbizwa Halmashauri ya Mji wa Bunda; tarehe 16 Agosti, 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Musoma, tarehe 17 Agosti, 2025 Manispaa ya Musoma na tarehe 18 Agosti, 2025  Halmashauri ya Butiama.

Tarehe 19 Agosti, 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Rorya; tarehe 20 Agosti, 2025 Halmashauri ya Mji wa Tarime; tarehe 21 Agosti, 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Tarime; tarehe 22 Agosti, 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti; na tarehe 23 Agosti, 2025 Halmashauri ya Wilaya ya Bunda.

Mhe. Mtambi amesema ukiwa Mara mwenge utakuwa umefika nyumbani na ukiwa katika Wilaya ya Butiama Mwenge wa Uhuru utatembelea nyumbani kwa Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na ukiwa hapo kama ilivyo kawaida utawasha Mwenge wa Mwitongo kwa mara ya 61 tangu mbio za Mwenge wa Uhuru zilipoanzishwa mwaka 1964.  

“Ninapenda kuwakaribisha wananchi wote wa Mkoa wa Mara na maeneo jirani kushuhudia kuwashwa kwa Mwenge wa Mwitongo kwa ajili ya kumuezi Baba wa Taifa na Muasisi wa Mwenge wa Uhuru tarehe 18 Agosti, 2025 kuanzia saa sita mchana.

Mhe. Mtambi ametumia fursa hiyo kuwaalika viongozi, watumishi wa Serikali, taasisi binafsi, mashirika yasiyo ya kiserikali, na wananchi wote kushiriki mbio za Mwenge wa Uhuru kwa kipindi chote utakapokuwa katika Mkoa wa Mara.

Aidha, Mhe. Mtambi amewahamasisha wananchi kushiriki kwenye Mbio za Mwenge wa Uhuru 2025 ili kupata ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru unaolenga kuwahamasisha na kuwaelimisha kushiriki kwenye uchaguzi Mkuu chini ya kauli mbiu isemayo “Jitokeze kushiriki Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2025 kwa Amani na Utulivu” utakaotolewa na Wakimbiza Mwenge Kitaifa wakiongozwa na Ndugu Ismail Ali Ussi, Kiongozi wa Mbio za Mwenge Kitaifa 2025. 

Announcements

  • MBIO ZA MWENGE WA UHURU, 2025 August 11, 2025
  • HAFLA YA UTIAJI SAINI MKATABA YA TACTICS August 11, 2025
  • KONGAMANO LA VIJANA August 11, 2025
  • MATOKEO YA MTIHANI WA KIDATO CHA NNE 2017 January 31, 2018
  • View All

Latest News

  • Mwenge wa Uhuru Wapitisha miradi 68 ya bilioni 26.5 Mara

    August 23, 2025
  • RC Mtambi akutana na viongozi wa dini na kuwasistiza kuhamasisha amani

    August 22, 2025
  • Wananchi Rorya wahimizwa kutumia nishati safi ya kupikia

    August 19, 2025
  • Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kitaifa awasha Mwenge wa Mwitongo kwa mara ya 61

    August 18, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.