Thursday 24th, April 2025
@Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Songe
Mheshimiwa Adam Kighoma Malima, Mkuu wa Mkoa wa Mara, anawaalika wadau wote wa Elimu wa Mkoa wa Mara kushiriki kwenye Kongamano la Wadau wa Elimu Mkoa wa Mara litakalofanyika katika ukumbi wa Shule ya Sekondari ya Wasichana ya Songe iliyopo Musoma tarehe 23 Februari 2020. Lengo la Kongamano ni kujadili na kuzipatia ufumbuzi changamoto za elimu za Mkoa wa Mara. Kongamano hili halina kulipa kiingilio. Michango ya hali na mali ya wadau kwa ajili ya maandalizi itapokelewa. Kwa mawasiliano kuhusu kongamano hilo wasiliana na Mwl. Elisonguo M. Mshiu-0756 437488 na Bw. Evance Sangawe- 0767 666363.
Wote Mnakaribishwa
Katibu Tawala Mkoa wa Mara
Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara
Telephone: +255282622305
Mobile:
Email: ras.mara@tamisemi.go.tz
Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.