• complaint |
    • Contact Us |
    • FAQ |
    • Staff Mail |
MARA REGION

The United Republic of Tanzania President's Office Regional Administration and Local Government MARA REGION

  • Home
  • About Us
    • History
    • Mission and Vision
    • Core Values
  • Administration
    • Organisation Structrure
    • Sections
      • Planning & Coordination
      • Education Sector
      • Water Services
      • Economic & Productive
      • Admin AND Human Resource Management
      • Health & Social Welfare
      • LGAs Management Services
      • Infastructure
    • Units
      • Legal Services
      • Finance & Accounts
      • Internal Audit
      • Information & Communication Technology
      • Procurement & Supply Management
  • District
    • Musoma District
    • Butiama District
    • Bunda District
    • Rorya District
    • Tarime District
    • Serengeti District
  • Council
    • Musoma Muncipal
    • Bunda DC
    • Bunda Town
    • Butiama DC
    • Rorya DC
    • Tarime DC
    • Tarime Town
    • Serengeti DC
    • Musoma DC
  • Investment Opportunities
  • Services
    • Water
    • Education
    • Health
    • Infastructure
    • ICT
  • Publications
    • Guidelines
    • Procedures
    • Reports
    • Policies
    • Application Forms
    • Integrity Pledge Form
    • Client Service Charter
  • Media Center
    • Press Release
    • Videos
    • Speeches
    • Photo Gallery
    • News
    • Events

Livestock

Kulingana na Sensa ya Watu na Makazi ya mwaka 2012 Mkoa unakadiriwa kuwa na jumla ya ng’ombe 1,651,355, mbuzi 757,428, kondoo 402,492 na kuku wapatao 1,612,672. Idadi kubwa ya mifugo hiyo inapatikana maeneo ya vijijini ni Ng’ombe 93%, mbuzi 95.6%, kondoo 97.5% na kuku 92.1% na mifugo mingine ikipatikana maeneo ya mijini. Mkoa wa Mara kuna livestock units 676,160 ambazo zinahitaji eneo la malisho Hekta 1,081,857. Eneo lililopo kwa ajili ya malisho ya mifugo ni hekta 750,000 hivyo kuna upungufu wa maeneo ya malisho hekta 405,697. Hii ina maana kwamba mifugo iliyopo katika Mkoa wa Mara ni mingi ukilinganisha na eneo la malisho lililopo.

Mkoa una hekta 43,170 ambazo zimetengwa na kupimwa kwa ajili ya malisho (Rorya ha 5,400, Bunda ha 743.2, Butiama ha 320, Musoma ha 150, Tarime ha 4,800 na Serengeti ha 31,757). Uendelezaji wa nyanda za malisho unafanyika zaidi kwa wafugaji wa ng’ombe wa maziwa ambao hutumia ufugaji wa ndani, kwa ng’ombe wa nyama uboreshaji unaenda taratibu kutokana na uchungaji huria. Mikakati ya kukabiliana na hali hii ni Serikali za Vijiji kuainisha matumizi bora ya Ardhi kwa kila Kijiji, kuendelea kuvuna mifugo na kuiuza minadani, kuboresha Koo safu za Mifugo, kuendelea kuelimisha wafugaji juu ya ufugaji wa ndani (zero grazing) pamoja na kutoa elimu ya ufugaji bora kwa wafugaji.

Kwa upande wa miundombinu ya mifugo Mkoa wa Mara una jumla ya Majosho 162 (64 mazima, 48 hayafanyi kazi, 43 yanahitaji ukarabati na 7 ni ya watu binafsi), Vibanio 82, Malambo 145 (135 mazima na 10 mabovu), Mabwawa 3, Minada 29, Vituo vya Afya ya Mifugo 33, Machinjio 28, Mashamba ya Mifugo 6, Vituo vya Kukusanyia Maziwa 22 na Matanki ya Kupozea Maziwa 3, Mabanda ya Ngozi 18, Holding Ground 1 na Mnada wa Upili 1. Uwepo wa miundombinu hii imesaidia katika kuongeza uzalishaji wa mazao yatokanayo na mifugo na hivyo kuboresha lishe na vipato vya wafugaji.

CHANGAMOTO

Pamoja na ustawi wa sekta ya Mifugo Mkoani bado kuna changamoto kadhaa zinazoathiri ukuaji na tija ya sekta hii ziwemo:-

  1. Uwepo wa magonjwa hatarishi ya mifugo ambayo yangeepukika kwa kuwepo wa kwa miundombinu bora na ya kutosha hususani majosho, madawa ya kuogeshea na madawa ya kinga na tiba mbalimbali.
  2. Kuendelea kumezwa kwa maeneo ya malisho katika jitihada za kupanua shughuli za kilimo na makazi.
  3. Malisho yasiyo bora. Kuenea kwa Jani Gugu –“Sporobolus Pyramidalis” katika Wilaya za Tarime, Serengeti, Musoma na Rorya na gugu vamizi aina ya “Chromoleana Oderata” maarufu kwa jina la “Amacha-bhongo” katika Wilaya za Serengeti, Tarime, Rorya, Butiama na Musoma Vijijini kumeleta changamoto.

 MIKAKATI YA KUKABILIANA NA CHANGAMOTO

Katika kukabiliana na changamoto mbalimbali, Mkoa umeweka mikakati ifuatayo:-

  1. Kutoa elimu pamoja na kuhamasisha wakulima kutumia miundombinu iliyopo ili kudhibiti magonjwa sambamba na kuhamasisha na kuelimisha vikundi kusimamia uogeshaji kwa kutumia miongozo iliyopo ili kupunguza migogoro kwenye vikundi vya wafugaji.
  2. Kutenga maeneo yatakayopandwa malisho bora na kutunzwa;
  3. Kuwa na Mipango ya matumizi bora ya Ardhi katika Vijiji; na
  4. Kuendelea Kushirikiana na Kituo cha Utafiti cha Mifugo – Mabuki katika mradi wa Utafiti juu ya Athari za Gugu vamizi aina ya Chromoleana oderata ulioanza Mwezi Novemba, 2015 kwa udhamini wa Tume ya Taifa ya Sayansi na Teknolojia (COSTECH).

Announcements

  • Ziara ya Waziri Mkuu February 24, 2024
  • MIAKA 60 YA MWENGE WA MWITONGO July 31, 2024
  • RC AIPOKEA KAMATI YA MADINI YA BUNGE February 25, 2024
  • SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA KIFO CHA WAZIRI MKUU MSTAAFU MHE. EDWARD LOWASSA February 11, 2024
  • View All

Latest News

  • Kongamano la Maonesho ya Madini kufunguliwa Mara leo

    June 03, 2025
  • Mtambi ataka ubunifu vyanzo vya mapato

    June 03, 2025
  • Mtambi aipongeza Musoma DC kupata hati safi

    June 03, 2025
  • Kusaya awataka wauguzi kuviishi viapo vyao

    May 30, 2025
  • View All

Video

UMUHIMU WA KULIPA KODI
More Videos

Quick Links

  • Huduma za Maji
  • Mpango wa Manunuzi wa mwaka wa fedha 2017/2018
  • FOMU ZA KUSAFIRI NJE YA NCHI
  • TAARIFA KWA MAKAMU WA RAIS
  • TAARIFA YA HOSPITALI YA WILAYA YA SERINGETI
  • Muongozo wa Matumizi bora ya vifaa vya TEHAMA
  • Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Mazingira duniani Mkoani Mara.
  • Zoezi la Unyunyiziaji Kiuatilifu cha Ukoko Majumbani
  • Taarifa kwa Umma-Ziara ya Makamu wa Rais Mkoa wa Mara

Related Links

  • IKULU
  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Tovuti Kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifu
  • Ofisi ya Rais-UTUMISHI
  • Idara ya Habari Maelezo

World visitors tracker

world map hits counter

Visitors Counter

writingMasterThesis

Location Map

Contact Us

    Katibu Tawala Mkoa wa Mara

    Postal Address: 13 Barabara ya Boma, P.o.Box 299 Musoma, 31101 Musoma, Mara

    Telephone: +255282622305

    Mobile:

    Email: ras.mara@tamisemi.go.tz

Other Contacts

   

    • Privacy Policy
    • Disclamer
    • FAQ
    • Sitemap

Copyright ©2017 Mara Region . All rights reserved.